Adnan Menderes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Adnan Menderes (1899 - 17 Septemba 1961) alikuwa mwanasiasa wa Uturuki. Alikuwa Waziri Mkuu wa Uturuki kati ya miaka 1950 na 1960.

Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Democrat (DP) mnamo 1946, chama cha nne kisheria cha upinzani cha Uturuki. Alihukumiwa na kunyongwa chini ya mamlaka ya kijeshi baada ya mapinduzi ya 1960, pamoja na wajumbe wengine wawili wa baraza la mawaziri, Fatin Rüştü Zorlu na Hasan Polatkan. Shtaka moja dhidi yake lilikuwa la yeye kuamuru Istanbul Pogrom dhidi ya raia wa kabila la Ugiriki.

Alikuwa kiongozi wa mwisho wa kisiasa wa Uturuki kunyongwa baada ya mapinduzi ya kijeshi na pia ni mmoja wa viongozi wa kisiasa wa Jamhuri ya Uturuki (pamoja na Kemal Atatürk na Turgut Özal) kujengwa kaburi kwa heshima yake.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adnan Menderes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.