Abby Chams
Abby Chams | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Abigail Chamungwana |
Amezaliwa | 2003 Tanzania |
Kazi yake | Mwanamuziki
|
Ameshirikiana na | wanamuziki mbalimbali kutoka ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania |
Abby Chams (anayejulikana sana kwa jina la kisanii kama Abigail Chams au Abigail Chamungwana) ni mwanaharakati wa kijamii, mpiga ala za muziki na mwimbaji kutoka nchini Tanzania.[1][2]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Abigail Chamungwana alizaliwa kwenye familia ya muziki; babu yake alikuwa kiongozi wa bendi ya muziki na bibi yake alikuwa mwimbaji wa kwaya kanisani.[3] Alianza kujifunza piano akiwa na umri wa miaka mitano na akajifunza kupiga fidla akiwa na miaka minane pia alijifunza kupiga gitaa, ngoma na filimbi.
Shuguli za kijamii
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 2020 Abby Chams aliteuliwa na UNICEF kuwa mtetezi wa vijana[4] nchini Tanzania kuhusu afya ya akili na usawa wa kijinsia wakati wa siku ya kimataifa ya watoto 2020; pia alitumbuiza katika maonyesho ya expo 2020 huko Dubai.[5]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 2022 Abby Chams alipendekezwa kuwania tuzo za Tanzania Music Awards kama msanii anayechipukia.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- Closer Ft Harmonize
- Tucheze
- Chapa rapa
- U&I
- Milele
- Nyash Ft S2kizzy, Dj Joozey
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Abby Chams The gospel voice fairy". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-10-22.
- ↑ "Waridi wa BBC: Abby Chams azungumzia changomoto za wanamuziki wa kike". BBC Swahili. Iliwekwa mnamo 2021-09-15.
- ↑ "Closer with Abigail Chams: KenyaBuzz Exclusive Interview". Kenya Buzz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-02.
- ↑ "[[UNICEF]] Appoints two new Youth Advocates during Expo 2020 Dubai ceremony". UNICEF (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-20.
{{cite web}}
: URL–wikilink conflict (help) - ↑ "Abby chams atumbuiza Expro2020 Dubai". Dar 24. Iliwekwa mnamo 2022-12-24.
![]() |
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Abby Chams kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |