2030 (wimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"2030"
Wimbo wa Roma Mkatoliki
Umetolewa 2012/2013
January, 2013
Umerekodiwa 2012
Aina ya wimbo Hip-hop ya Tanzania
Lugha Kiswahili
Urefu 6:30
Studio Tongwe Records
Mtunzi Roma Mkatoliki
Mtayarishaji Jay Rider

2030 ni jina la wimbo uliotungwa na kuimbwa na msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Roma Mkatoliki. Wimbo ulirekodiwa mnamo mwaka wa 2012 kupitia studio ya Tongwe Records chini ya utayarishaji wake Jay Rider. Kama jinsi ilivyo kawaida ya Roma, wimbo unalenga masuala ya kijamii zaidi kuliko habari za starehe. Maelezo ya ndani yanabashiri au kutazamia namna Tanzania ya 2030 jinsi itakavyo kuwa. Hasa anaponda sera za serikali ya CCM namna inavyoendesha nchi na huu mmong'onyoko wa udini unaoendelea kuikumba Tanzania kwa kipindi hiki.

Katika wimbo, ametaja mauaji ya Mapadri na Masheikhe. Hina haja ya kutukana Quran wala Biblia. Anaimba kwa amani zote kuhakikisha ya kwamba haiegemei upande wa mtu yeyote ndani yake.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]