Wilaya ya Ludewa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Ludewa (kijani) katika mkoa wa Iringa kabla ya umegaji.
Wilaya ya Ludewa ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Njombe.
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 128,520 [1].
Ludewa iko upande wa kaskazini-mashariki ya Ziwa Nyassa. Makao makuu ni mji wa Ludewa. Wilaya imepakana na wilaya za Njombe na Makete, upande wa mashariki na mkoa wa Ruvuma na upande wa kusini na nchi ya Malawi ng'ambo ya ziwa.
Wenyeji asilia wa Ludewa ni Wapangwa, Wakisi na Wamanda.
| Kata za Wilaya ya Ludewa - Tanzania | ||
|---|---|---|
|
Ibumi | Iwela | Kilondo | Luana | Ludende | Ludewa | Lugarawa | Luilo | Lumbila | Lupanga | Lupingu | Madilu | Madope | Makonde (Ludewa) | Manda (Ludewa) | Masasi (Ludewa) | Mavanga | Mawengi | Milo | Mkomang'ombe | Mlangali (Ludewa) | Mundindi |
||