Manda (Ludewa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mbuyu mkubwa karibu na bandari ya Manda (Picha na Chemi Che Mponda)
Kata ya Manda
Nchi Tanzania
Mkoa Iringa
Wilaya Ludewa
Idadi ya wakazi
 - Mji 8,084

Manda ni jina la kata ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Iringa, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 8,084 waishio humo. Zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilijulikana kwa jina la Wiedhafen [1] ikawa kitovu cha Nyassa ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Wajerumani walichagua mahali pa Wiedhafen-Manda kwa sababu ilikuwa mwisho wa njia ya misafara kati ya Kilwa na Ziwa Nyassa na kuwa na bandari asilia.

Manda iko kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa karibu na mdomo wa mto Ruhuhu, ina vivutio vingi ikiwemo ufukwe maridhawa wa ziwa Nyasa. pia kuna Kanisa la Mt Thomaso na pia bandari ya kale ya Manda-Wiedhafen.

Wenyeji wa kata ya Manda ni wamanda na lugha yao ya asili ni kimanda. Vyakula vya asili vya wakazi wa Manda ni Ugali wa muhogo na samaki. Ngoma za asili za wakazi wa Manda ni Mganda, Kihoda na ligambusi. [2]

Marejeo [hariri]

  1. ling. Makala Wiedhafen katika Koloniallexikon ya 1920
  2. 2002 Population and Housing Census General Report (en). Government of Tanzania. Rudishwa juu ya 2008-08-21.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Ludewa - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Ibumi | Iwela | Kilondo | Luana | Ludende | Ludewa | Lugarawa | Luilo | Lumbila | Lupanga | Lupingu | Madilu | Madope | Makonde (Ludewa) | Manda (Ludewa) | Masasi (Ludewa) | Mavanga | Mawengi | Milo | Mkomang'ombe | Mlangali (Ludewa) | Mundindi


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Manda (Ludewa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.