Vijana jazz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Vijana Jazz (pia wanajulikana kama Vijana Jazz Band au Vijana Jazz Orchestra) ni bendi ya muziki wa dansi ya Kitanzania. Bendi hiyo ilifikia upeo wa umaarufu wao katika miaka ya 1980. Vijana Jazz, kama bendi nyingi za dansi za nyakati hizo, ilifadhiliwa na taasisi ya serikali – Umoja wa Vijana. Umoja wa Vijana ulikuwa mrengo wa vijana wa chama tawala cha Tanzania – Tanganyika African National Union.[1] Wanamuziki mashuhuri ambao wamecheza katika Vijana Jazz ni Hamza Kalala, Hemedi Maneti, Issa Chikupele, na Manitu Musa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Bendi ilianzishwa mnamo mwaka elfu moja mia tisa sabini na moja na John Ondoro Chacha. Miaka miwili baada ya kuanzishwa, Vijana Jazz ilijiunga na mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Hemedi Maneti.[2] Maneti alichukua jukumu kubwa katika kuongoza bendi hiyo na aliendelea kuongoza bendi hiyo kutoka mwaka elfu moja mia tisa themanini na mbili hadi kifo chake mwaka elfu moja mia tisa na tisini.[2] Walikuwa moja ya bendi ya kwanza kuchukua faida ya sheria iliyopitishwa na serikali ya Tanzania inayoruhusu bendi kununua vyombo vya muziki vya kigeni. Kabla ya sheria kupitishwa mnamo mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na nane, ununuzi wa vyombo vya muziki vya kigeni ulipigwa marufuku na Baraza la Muziki la Kitaifa - baraza la serikali linalohusika na kusimamia biashara ya muziki.[3] Vijana Jazz alichukua fursa huo na kuwa maarufu sana mwaka wa elfu moja mia tisa na themanini baada ya kuunda sauti mpya za ubunifu kwa kutumia synthesizers na ngoma za elektroniki.

Nchini Tanzania, bendi za muziki za dansi ziliunda mitindo ya muziki inayoitwa mtindo. Saini mtindo wa 'ijana Jazz ilikuwa kamata sukuma lakini pia walijulikana kwa koka koka. Mbalimbali mtindo ya Vijana Jazz na bendi ya muziki wa dansi mwingine ulipoteza umaarufu wakati wa miaka ya elfu moja mia tisa na themanini wakati fomu ya serikali ya Tanzania, inayojulikana kama Ujamaa, ilianza kufeli. Nchi ilipata uvumbuzi wa kiuchumi, na serikali haikuweza kulipa wanamuziki tena.[3]

Vijana Jazz nchini Kenya[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka ya elfu moja mia tisa na sabini, Kenya na Tanzania walikuwa washirika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na wanamuziki wa Kenya na Tanzania wangeweza kusafiri kwa uhuru kati ya nchi kufanya kazi.[2] Muziki wa Tanzania ulikuwa maarufu nchini Kenya na bendi za Kitanzania, kama Vijana Jazz, mara nyingi zilifanya safari ya saa ishirini na nne kutoka Dar es Salaam mpaka Nairobi kucheza na kurekodi muziki.

Vijana Jazz walianza kurekodi muziki wao katika Polygram Records Kenya na A.I.T Records jijini Nairobi kwa sababu  kama bendi zingine nyingi za muziki wa dansi zilikuwa na uhusiano mbaya na Radio Tanzania Dar es Salaam.[3] Katika miaka ya elfu moja mia tisa na sabini, Radio Tanzania Dar es Salaam ilikuwa studio pekee ya kurekodi nchini Tanzania. Bendi nyingi za muziki wa dansi zilisusia Radio Tanzania Dar es Salaam kwa sababu walijifunza rekodi zao ambazo zilikuwa za ujambazi na kutolewa Kenya. Bendi hizo hazikupokea malipo yoyote kwa rekodi zao. Pia, bendi hazikuwa na mipango ya mkataba, kwa hivyo wanamuziki hawakuweza kufuata mauzo ya muziki wao.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Askew, K. M. (2002). Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics in Tanzania. Chicago: University of Chicago Press.
  2. 2.0 2.1 2.2 Williams, S. (2011, December 18). Sex Batillion: The Koka Koka. Retrieved from African Business: https://african.business/2011/12/economy/sex-battalion-the-koka-koka/
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Odidi, B. (2016, March 29). Tanzania as an East Africa musical powerhouse. Retrieved from Music in Africa: https://www.musicinafrica.net/magazine/tanzania-east-african-musical-powerhouse