Muziki wa dansi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Muziki wa dansi (au dansi tu) ni muziki kutoka nchini Tanzania. Ulianzishwa katika mji wa Dar es Salaam kunako miaka ya 1930, na unapendeka leo hadi leo hii.

Muziki wa dansi unatokana na muziki wa soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (au "rumba ya kikongo") na tokea hapo ikawa inaitwa "rumba ya Tanzania" pia.

Kwa kawaida, maneno ya nyimbo ya muziki wa dansi ni kwa lugha ya Kiswahili tokea hapo awali na pia dansi huitwa "swahili jazz" kwa lugha ya Kiingereza.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa Ujerumani na Uingereza[hariri | hariri chanzo]

Ukitaka kuongea muziki wa dansi uliingiaje nchini ni muhimu kujua historia ya mji wa Tanga. Tanga ndipo muziki wa dansi ulipoingilia nchini. Wajerumani waliusambaratisha mji wa Tanga kwa mizinga kati mwaka 1888 na 1889. Na baada ya hapo kuujenga upya kwa kufuata mpangilio uliosababisha Tanga kuwa na mitaa maarufu kama barabara ya kwanza ya pili na kuendelea. Wajerumani walianzisha shule ya kwanza ya serikali Tanga 1892 na hapohapo wakanzisha bendi ya shule ya kwanza, pamoja na kuwa Wajerumani hawakutawala muda mrefu baada ya hapo lakini Waingereza waliiendeleza sana bendi hiyo iliyokuwa ikipiga aina mbalimbali za muziki wa kigeni.


Dansi ilianza kwanza kama klabu ambapo watu walialikana kuja kucheza aina mbalimbali za muziki wa kizungu mtindo maarufu unaojulikana kama ballroom dancing. Aina hizi za klabu zilianzia Mombasa na kuingia nchini kupitia Tanga na kisha kuletwa Dar Es Salaam na klab iliyokuwa maarufu Tanga iliyoitwa Tanga Young Comrades Club, klabu nyingine ilianzishwa ikaitwa New Generation Club ambayo ilianzisha matawi miji mbalimbali. Klabu hizi ndizo zilizozaa bendi za dansi. Inaonekana Dar Es Salaam ndio ilikuwa ya kwanza kuwa na bendi yake African Association Jazz Band, ambapo wanamuziki wengine waliihama na kuanzisha Dar Es Salaam Jazz Band, hiki kilikuwa kipindi kati ya miaka 1930 na 1940, kwenye 1950 kulikuwa na bendi maarufu Bagamoyo iliyoitwa Lucky Star jazz band ambayo ilikuwa na urafiki na Dar Jazz.


Baada ya hapo kulianza bendi ambazo wanamuziki na wanachama wake walipatikana kutokana na wanakotoka, kulikuweko na Ulanga Jazz band ya Wapogolo, Rufiji Jazz Band iliyoanzishwa na Wandengeleko, Western Jazz iliyoanzishwa kwanza na Wanyamwezi. Bendi zote hizi baadae zilikuja kuwa na wanachama mchanganyiko bila kujali uzawa. Na kulikuweko na Skokian Jazz Band hii ilikuwa ni bendi na klabu ya watu mchanganyiko. Mwaka 1958 wanamuziki kutoka Kilwa walianzisha Kilwa Jazz Band wanamuziki hawa walitoka bendi iliyoitwa Tanganyika Jazz.[1]

Ilipofika 1966 bendi ilikuwa na wanamuziki takribani 26, 15 wakiwa Kilwa A na 11 Kilwa B. Zamani bendi zilikuwa na mtindo wa kuwa na bendi B ambayo ni ya Vijana. Patrick Balisdya aliwahi kuwa Dar Jazz B. Kilwa Jazz ilikuwa na wanachama kama 50 wengine wakiwa viongozi wa juu serikalini. Waliolipa ada ya uanachama na hivyo kuweza kuingia madansi ya bendi bila kulipa. Wakati huo makao makuu ya Kilwa Jazz yalikuwa katika ukumbi ambao kwa sasa unaitwa Kwa Madobi maeneo yaa Jangwani.

Katika miaka ya 1920[hariri | hariri chanzo]

Muziki ulianzishwa kunako miaka ya 1920-1930, zikiwa na mandhari ya muziki wa "soukous" kutoka Kongo-Kinshasa, kwa kweli zilipendeka kote Afrika ya Mashariki. Katika Dar es Salaam, bendi nyingi zilifuatisha bendi za Kongo. Punde kwa punde, zingine ziliendeleza kuanzisha mitindo mipya, kwa mfano Dar es Salaam Jazz Band, Morogoro Jazz na Tabora Jazz.

Baada ya uhuru wa Tanzania, bendi nyingi za muziki wa dansi nilitegemea ofisi au vyama. Kwa mfano, NUTA Jazz Band ilikuwa bendi bayana na ilitegemea Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania ("National Union of Tanzania", NUTA, kwa Kiingereza).

Kunako miaka ya 1960-1980 muziki wa dansi uliendelea kwa ajili ya bendi bayana kama Orchestra Safari Sound, Orchestra Maquis Original, International Orchestra Safari Sound, DCC Mlimani Park Orchestra na Vijana Jazz. Baadhi ya bendi kisasa ni Gari Kubwa, Tokyo Ngma na Atomic Advantage.

Hulka[hariri | hariri chanzo]

Bendi nyingi za muziki wa dansi zilicharaza kila usiku, katika vilabu, mahoteli na kadhalika, na wanamuziki walipokezana. Kwa mfano Morogoro Jazz ilicharaza katika hoteli ya "Morogoro Hotel" ya Morogoro. Pia wanamuziki walikuwa wakifanyakazi kwa kulipwa, na bendi ilikuwa imikimiliki vyombo vya muziki. Wanamuziki mashuuri walibadili bendi mara nyingi, hata kuchuma zaidi na hatimaye kuanzilisha bendi zao. Kwa mfano Muhiddin Maalin na Hassani Bitchuka walicharaza katika mabendi mengi.

Kila bendi huwa na mtindo unatambulikana, na mwanamuziki hujikaribisha kwa mtindo wa bendi yao baada ya kuajiriwa. Kwa kawaida jina la mtindo larejea gungu, kwa mfano ogelea piga mbizi ya Orchestra Maquis Original. Wasanii wengine hujulikana kwa sababu huweza kuunda mitindo vizuri.

Kwa kawaida, nyimbo wa muziki wa dansi huanza polepole kusisitiza maneno na mwimbaji; kisha, hatua kwa hatua hukuwa haraka (kipande hiki huiitwa chemko), na ngoma na magitaa huongeza kwa sauti.

Ushindani baina ya bendi kubwa ni muhimu kwa muziki wa dansi. Kwa mfano, Orchestra Maquis Original hushindana na Orchestra Safari Sound (kunako miaka ya 1970-1980) na baadaye International Orchestra Safari Sound hushindana na Mlimani Park. Sherehe za muziki wa dansi hufanywa kama shindano pia.

Bendi maarufu[hariri | hariri chanzo]

Jina Pia inajulikana kama Kipindi/Miaka ya Mahali Mitindo Wanamuziki maarufu
Dar es Salaam Jazz Band Dar Jazz 1930-1970 Dar es Salaam Michael Enoch
Morogoro Jazz Band Morogoro Mbaraka Mwinshehe, Salim Adballah
NUTA Jazz Band Juwata Jazz Band, OTTU Jazz Band 1960- Joseph Lusungu, Mnenge Ramadhani, Muhiddin Maalim, Hassani Bitchuka, Saidi Mabera, Abel Balthazar
Orchestra Maquis Original 1970- Dar es Salaam kamanyola, zembwela Chinyama Chianza, Nguza Mbangu, Dekula Kahanga
Orchestra Safari Sound 1970-1985 Ndala Kasheba
Mlimani Park Orchestra 1978-? sikinde Muhiddin Maalim, Hassani Bitchuka, Abel Balthazar, Michael Enoch, Cosmas Chidumule, Shaaban Dede, Maalim Kinyasi
Vijana Jazz 1980-1990
International Orchestra Safari Sound IOSS 1985-? ndekule Muhiddin Maalim, Hassani Bitchuka, Abel zBalthazar, Nguza Mbangu

Zahir ally

zolo

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Historia ya muziki wa dansi katika Blogu ya Anko John Kitime