Uti wa mgongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
- Uti wa mgongo katika mwili wa kibinadamu
Sehemu za uti wa mgongo

Uti wa mgongo ni nguzo ya mifupa ambayo ni kiini cha kiunzi cha mifupa katika miili ya vetebrata kama binadamu, mamalia wote na pia wanyama wengine wengi kama samaki, reptilia na ndege.

Kazi ya uti wa mgongo[hariri | hariri chanzo]

Nguzo hii ya uti wa mgongo inashikamanisha mifupa yote kwa pamoja kuanzia fuvu na mabavu hadi mifupa ya chini inayokutana katika fupanyonga.

Pamoja na kuwa kiini cha kiunzi cha mifupa, uti wa mgongo huwa na kazi ya pili muhimu: inatunza ndani yake neva za ugwemgongo zinazofikisha amri za ubongo mwilini mwote. Neva za ugwembongo ni nyeti sana; hivyo uharibifu kwenye uti wa mgongo unaoathiri neva hizo kiasi unaweza kusababisha maumivu makali au hata ulemavu kama neva zinakatika na sehemu za mwili hazipokei tena amri kutoka ubongo.

Sehemu za uti wa mgongo[hariri | hariri chanzo]

Uti wa mgongo unafanywa na pingili au vetebra 33-35, kutegemeana na umri wa mtu; tofauti hutokea kwenye sehemu ya kifandugu. Pingili 24 za juu zinatenganishwa na visahani vya vetebra. Huangaliwa na matibabu kuwa sehemu kuu tano:

  • Uti wa shingoni (ing. cervical, lat. pars cervicalis) : inashika fuvu la kichwa (nyekundu). Ina pingili 7. Mbili za juu zinaunganisha fuvu na uti wa mgongo.
  • Uti wa kifuani (ing. thoracic, lat. pars thoracica): sehemu hii (buluu) inashika mabavu yote mahali pake. Ina pingili 12.
  • Uti wa kiuno (ing. lumbar, lat. pars lumbalis): sehemu hii inaunganisha mwili wa juu na mwili wa chini. Inamwezesha mwanadamu kugeuza mwili bila kusogeza miguu. Ina pingili 5 (njano).
  • Uti wa nyonga (ing. sacrum, lat. os sacrum) inashika nyonga. Ni pingili tano ambazo kwa kawaida zimeungana kama mfupa mmoja - (kibichi)
  • Kifandugu (ing. coccyx) - inashika misuli kadhaa (zambarau), ina pingili 3-5.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uti wa mgongo kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.