Urani
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Urani (uranium) |
|
|---|---|
|
|
|
| Jina la Elementi | Urani (uranium) |
| Alama | U |
| Namba atomia | 92 |
| Mfululizo safu | Metali |
| Uzani atomia | 238.0289 |
| Valensi | 2, 8, 18, 32, 21, 9, 2 |
| Densiti | 19.1 g·cm³ |
| Kiwango cha kuyeyuka | 1405.3 K (1132.2 °C) |
| Kiwango cha kuchemka | 4404 K (4131 °C) |
| Asilimia za ganda la dunia | 3 · 10-4 % |
| Hali maada | mango |
Urani ni elementi katika mfumo radidia yenye alama U. Namba atomia ni 92 na uzani atomia ni 238. Jina limechaguliwa kutokana na sayari Uranus.
Urani ni metali nururifu. Isotopi yake 235U ni dutu asilia ya pekee inayoweza kuwa na mmenyuko mfululizo wa kinyuklia. Hutumiwa katika tanuri nyuklia pia katika silaha za nyuklia. Bomu ya nyuklia ya kwanza huko Hiroshima ilitengenezwa kwa Urani.
[hariri] Umuhimu wa kiuchumi
Ikiwa ni metali nururifu ya pekee inayopatikana duniani kiasili hutumiwa kwa utengenezaji wa umeme katika tanuri nyuklia. Takriban asilimia 16 ya umeme duniani hutengenezwa kwa njia hii, katika nchi kadhaa ni sehemu kubwa ya umeme. Mwanzoni wa upatikanaji wa teknolojia hii katika karne ya 20 kulikuwa na matumaini makubwa ya kuwa italeta umeme nafuu kwa watu wote. Ila tu matatizo ya takataka nyuklia na ajali hatari za tanuri nyuklia yalichelewesha maendeleo ya matumizi yake. Tena upatikanaji wa urani yenyewe ni tatizo kwa sababu akiba za urani duniani zinazofaa kwa uchimbaji wa kiuchumi hukadiriwa kudumu kwa miaka 50-100 pekee.
| Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Urani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Urani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |