Ununbi
| Ununbi (Ununbium) |
|
|---|---|
| Jina la Elementi | Ununbi (Ununbium) |
| Alama | Uub |
| Namba atomia | 112 |
| Mfululizo safu | matali za mpito (?) |
| Uzani atomia | 277 g/cm³ (kadirio) |
| Valensi | 2, 8, 18, 32, 32, 18, 2 |
| Asilimia za ganda la dunia | 0% (elementi sintetiki) |
| Hali maada | huaminiwa kuwa gesi au kama metali |
| Mengineyo | Ununubi ni elementi sintetiki yenye nusumaisha mafupi sana iliyotengenezwa mara nne tu |
Ununubi ni elementi sintetiki yenye namba atomia 112 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 277. Alama yake ni Uub. Si rahisi kutaja tabia zake kwa sababu imetengenezwa mara nne tu katika maabara kama atomi moja-moja.
Yaliyomo |
[hariri] Jina
Jina latokana na maneno ya kilatini kwa "1" (unum) na kwa "2" (bi). Un-un-bi yamaanisha hivyo moja-moja-mbili yaani namba atomia ya elementi. Ununbi ni jina la muda inawezekana ya kwamba jina lingine litatolewa kama wataaalamu hukubaliana.
[hariri] Ufumbuzi
Elementi iliwahi kutabiriwa na wanasayansi kuwa inaweza kupatikana. Ilitengenezwa mara ya kwanza 1996 na wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Darmstadt kwa kufyatulia viini vya atomi za zinki katika risasi.
[hariri] Matumizi
Kama elementi zote za sintetiki haina matumizi bado zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena. Kuna uwezekano ya kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu kutokana na maisha mafupi ya atomi zao zimeshapotea muda mrefu.