Elementi sintetiki
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elementi sintetiki ni elementi za kikemia ambazo haitokei kiasili duniani bali zinaweza kutengenezwa katika maabara. Zinaitwa pia transurania kwa sababu ziko nzito kushinda urani ambayo ni elementi nzito inayopatikana duniani kiasili.
Hazipo kiasili kwa sababu si imara kutokana na nusumaisha fupi mno; kama zilipatikana kutokana na mmenyuko wa kinyuklia asilia zilipotea tayari tangu muda mrefu. Muda wa maisha ya elementi sintetiki ni kati ya sekunde (au sehemu za sekunde tu) hadi miaka kadhaa. Zote ni nururifu yaani zinatoa mnururisho wa kinyuklia.
Elementi sintetiki [hariri]
- Transurania
- Ameriki alama Am, namba atomia 95
- Kuri alama Cm, namba atomia 96
- Berkeli alama Bk, namba atomia 97
- Kaliforni alama Cf, namba atomia 98
- Einsteini alama Es, namba atomia 99
- Fermi alama Fm, namba atomia 100
- Mendelevi alama Md, namba atomia 101
- Nobeli alama No, namba atomia 102
- Lawirensi alama Lr, namba atomia 103
- Rutherfordi alama Rf, namba atomia 104
Majina ya muda kwa elementi sintetiki zilizopatikana juzi tu