Tetemeko la ardhi la Kagera 2016

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tetemeko la ardhi la Kagera 2016 is located in Tanzania
Tetemeko la ardhi la Kagera 2016
Mahali pa tetemeko la ardhi la 2016 Kagera, Tanzania

Tetemeko la ardhi kwenye Mkoa wa Kagera lilianza kutokea tarehe 10 Septemba mwaka 2016 karibu na mji wa Bukoba nchini Tanzania.

Zilizala hii, iliyopimwa kuwa na nguvu ya 5.9 kwenye skeli ya MMS, ikatokea takriban kilomita 40 chini ya uso wa ardhi katika mazingira ya kata ya Nsunga karibu na mpaka kati ya Tanzania na Uganda[1].

Mshtuko ulisikika hadi Uganda, Burundi, Rwanda, Jamhuri ka Kidemokrasia ya Kongo na Kenya.[2][3]

Nchini Tanzania watu 16 waliripotiwa kufa na 203 kujeruhiwa, hasa mjini Bukoba ambako shule moja iliporomoka[4] na watu 4 walikufa kwenye kata ya Kamuli.

Taarifa za wajeruhiwa zimefika pia kutoka Uganda wakati nyumba iliporomoka katika wilaya ya Rakai.[5]

Mjini Bukoba zaidi ya nyumba 270 ziliharibiwa. Katika Uganda eneo lililoathiriwa zaidi ni Kyebe pamoja na Minziiro na Kannabulemu.[6]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "M5.9 - 22km NE of Nsunga, Tanzania". United States Geological Survey. September 10, 2016. Iliwekwa mnamo September 10, 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "5.7 earthquake hits northwest Tanzania, 11 dead and many injured". Africanews. September 10, 2016. Iliwekwa mnamo September 10, 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "Tanzania rocked by 5.7 magnitude earthquake", September 10, 2016. Retrieved on September 10, 2016. 
  4. "Tanzania earthquake toll clims to 14 dead, 200 injured". Korea Herald. September 11, 2016. Iliwekwa mnamo September 11, 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. "Lives lost, houses collapse as earthquake hits Uganda". The Observer. September 10, 2016. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-11. Iliwekwa mnamo September 11, 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. "Ten killed in Tanzania earthquake". Deutsche Presse Agentur. September 10, 2016. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-11. Iliwekwa mnamo September 10, 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)