Tekineti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Tekineti (Technetium)
Tekineti (ubamba)
Jina la Elementi Tekineti (Technetium)
Alama Tc
Namba atomia 43
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 98
Valensi 2, 8, 18, 13, 2
Densiti 11
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 2430 K (2157  °C)
Kiwango cha kuchemka 4538 K (4265 °C)
Hali maada mango
Mengineyo Tekineti ni nururifu; nusumaisha ya isotopi zake ni kati ya miaka 211 hadi miaka milioni 4.2

Tekineti (kutoka Kigiriki τεχνητός teknitos "bandia") ni elementi sintetiki na metali. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Tc na namba atomia 43 katika mfumo radidia.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Tekineti hupatikana kwa maumbo mbalimbali. Ikitokea kama vumbi ina rangi ya majivu. Ikitokea kama metali imara hufanana na platini.

Ni elementi nururifu inayopatikana kwa kawaida kama elementi sintetiki inayotengenezwa kwa matumizi yake. Hutokea pia kiasili kwa viwango vidogo sana katika mbunguo wa urani.

Isotopi[hariri | hariri chanzo]

Isotopi inayopatikana zaidi ni 99mTc yenye nusumaisha ya miaka 211. Hutumiwa katika tiba kwa uchunguzi wa mwili hasa uaguzi wa kansa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kuwepo kwa elementi hii kulitabiriwa na Mendeleev tangu karne ya 19. Ilitambuliwa mara ya kwanza 1925 Ujerumani lakini jaribio halikuweza kurudiwa.

Mwaka 1937 ilipatikana kwa njia iliyokubaliwa na umma wa sayansi kwenye chuo kikuu cha Palermo (Sisilia - Italia). Emilio Segrè na Carlo Perrier walipata elementi mpya katika ubamba wa Molibdeni uliowahi kupigwa kwa mnururisho wa kinyuklia. Hii ilikuwa elementi sintetiki ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu. Wafumbuzi wakatoa jina la "technetium" kutokana na neno la Kigiriki kwa "bandia".


Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tekineti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.