Somaliland
|
|||||
| Wito la taifa: لا إله إلا الله محمد رسول الله (kar.) Lā ilāhā illā-llāhu; muhammadun rasūlu-llāhi (transliteration) "Hapana Mungu isipokuwa Allah tu, Muhammad ni mtume wa Allah" Pia : "Justice, Peace, Freedom, Democracy and Success for All" |
|||||
| Wimbo wa taifa: Saamo ku waar | |||||
![]() |
|||||
| Mji mkuu | Hargeisa (1941-1960) (1991 - present) |
||||
| Mji mkubwa nchini | Hargeisa | ||||
| Lugha rasmi | Kisomalia, Kiarabu na Kiingereza | ||||
| Serikali
Rais
Makamu wa Rais |
Jamhuri Ahmed M. Mahamoud Silanyo Abdirahman Saylici |
||||
| Uhuru kutoka Jamhuri ya Somalia |
18 Mei 1991 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
137,600 km² ({{{area_rank}}}) n/a |
||||
| Idadi ya watu - 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
3.5 millioni (n/a) 25/km² (n/a) |
||||
| Fedha | Shilingi ya Somaliland (SLSH) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EAT (UTC+3) - (UTC+3) |
||||
| Intaneti TLD | - | ||||
| Kodi ya simu | +252 [imependekezwa 292]
- |
||||
Somaliland (Kisomalia: Soomaaliland) ni jamhuri ya kujitawala katika kaskazini ya eneo la Somalia. Hali halisi ni nchi huru tangu 1991 lakini haikutambuliwa na umma wa kimataifa. Eneo lake ni sawa na koloni ya zamani ya Somalia ya Kiingereza jumla kilomita za mraba 137,600 iliyokuwa nchi huru kwa siku chache mwaka 1960 kabla ya kuungana na Somalia ya Kiitalia.
Imepakana na Ethiopia, Djibouti, Ghuba ya Aden na jimbo la Puntland la Somalia. Mji mkuu wa Somaliland ni Hargeisa.
Wakazi[hariri]
Kuna wakazi milioni 3.5. Zaidi ya nusu ni wafugaji wahamiaji na takriban 45 % hukaa mjin i au vijijini. Karibu wote ni Wasomalia hasa wa kabila ka Isaaq, wengine ni wa Dir au Darood.
Historia[hariri]
Habari za kwanza zinazojulikana kuhusu eneo la Somaliland zasema lilikuwa chini ya milki ya Axum na na baadaye Usultani wa Adal. Bandari ya Berbera ilijulikana tangu zamani za Periplus ya Bahari ya Eritrea.
Katika karne ya 16 Waosmani waliingia wakishika utawala juu ya sehemu za magharibi kwa sbabu walitaka kusimamia mlango wa Bahari ya Shamu Bab el Mandeb.
Walifuatwa na Misri na baadaye Uingereza. Waliitawala kama "British Somaliland Protectorate" au eneo lindwa la Somalia ya Kiingereza.
Koloni ikapewa uhuru wake tar. 26 Juni 1960 kama Nchi ya Somaliland ikaungana baada ya siku tano na Somalia ya Kiitalia kuwa Jamhuri ya Somalia.
Wakati wa udikteta wa Siad Barre watu wa kabila la Isaaq waliteswa sana wakaanza kuchukua silaha dhidi ya raisi huyu. Baada ya kuporomoka kwa serikali yoyote nchini Somalia wazee wa eneo lililokuwa SOmaliland walikutana na kuamua kurudisha uhuru wa awali.
Viungo vya Nje[hariri]
| Nchi za Afrika | |
|---|---|
| Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
| Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
| Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Somaliland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
