Shati ya Madiba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nelson Mandela mwaka 1998, akiwa amevalia shati la Madiba

Shati ya Madiba, ni shati la hariri , kwa kawaida hupambwa kwa uchapishaji wa rangi. Lilijulikana katika miaka ya 1990, wakati Nelson Mandela alipochaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini wakati huo alipoongeza kipengee hicho kwenye vazi lake la kawaida. Mandela alieneza aina hii ya shati, na kuinua vazi lililoonekana kuwa la kawaida katika hali rasmi.

Uundaji[hariri | hariri chanzo]

Aina ya mavazi ya kawaida, Mashati ya Madiba yanalegea, kwa kawaida huvaliwa bila tai na kufunguliwa kutoka kwa suruali. Limetolewa kutokana na nguo za batiki za Kiindonesia, na kwa ujumla hutengenezwa kwa pamba au hariri iliyochorwa kwa rangi angavu [1]. Mandela alisemekana kupendelea rangi za udongo kwa shati, ingawa mashati ya Madiba yenye rangi angavu yamedumu kwa umaarufu [2].

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kuna wengi wanaodai uvumbuzi wa shati la Madiba . Lakini ukweli ni kwamba, kulingana na Yusuf Surtee, mmiliki wa duka la nguo ambaye alimpa Mandela mavazi kwa miongo kadhaa, alisema muundo wa Madiba unatokana na ombi la Mandela la kumpa shati kama vazi la batiki la Rais wa Indonesia Suharto. Mbunifu wa mitindo Desré Buirski aliwasilisha aina hii ya shati kwa Mandela kama zawadi tarehe 7 Mei 1994 kwa kuipata kwa mlinzi wakati wa kutembelea sinagogi la Cape Town; Mandela alivaa shati hilo kwenye mazoezi ya kuapishwa kwake urais. [4][1] Sonwabile Ndamase alisema "alikuwa wa kwanza kulivaa" mnamo 1990.[3]

Mandela alivaa shati la aina hii mara kwa mara, ambalo lilijulikana kama "shati za Madiba ", lilipewa jina la ukoo wa Mandela wa Xhosa [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maynard 2004, Imewekwa Mnamo 19 - 03 - 2022
  2. Smith 2014, Immewekwa mnamo 19 - 03 -2022
  3. Smith 2014, Imewekwa mnamo 19 - 03 - 2022
  4. Grant & Nodoba 2009 Imewekwa mnamo 19 - 03 - 2022.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shati ya Madiba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.