Sera za kigeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rais Trump wa Marekani na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini walikutana Singapur mwaka 2018 katika jaribio la kubadilisha sera za kigeni kati ya mataifa yao.

Sera za kigeni ya nchi (pia inaitwa sera ya mahusiano ya kimataifa, siasa ya nje; kwa Kiingereza: foreign policy) ni jumla ya matendo, matamko na mipango ya nchi vinavyolenga kuendeleza uhusiano wake na nchi nyingine, pamoja na jumuiya na mashirika vya nchi za nje kuhusu uchumi, siasa, jamii na jeshi.

Sera za kigeni zinabuniwa ili kusaidia kulinda maslahi ya taifa, usalama wa taifa, malengo ya kiitikadi, na mafanikio ya kiuchumi. Hii inaweza kufanyika kama matokeo ya ushirikiano wa amani na mataifa mengine, au kwa njia za kutisha hadi kutumia nguvu ya kijeshi.

Kwa kawaida sera ya kigeni huongozwa na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje. Katika baadhi ya nchi bunge pia lina jukumu kiasi la kuzisimamia.

Katika nchi mbalimbali, hasa zenye Serikali ya kiraisi, mkuu wa nchi ana jukumu kwa sera za kigeni, wakati mkuu wa serikali hasa anahusika na sera ya ndani.

Nadharia ya mahusiano ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Taaluma inayoshughulika na utafiti wa mahusiano ya kigeni hujulikana kama uchambuzi wa sera za kigeni (Foreign Policy Analysis).

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]