Sans Commentaire ni jina la kutaja albamu ya mwimbaji wa muziki wa dansi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo maarufu kama Madilu System. Albamu imetoka mwaka wa 1994. Utayarishaji wa albamu hii ulifanyika nchini Ufaransa katika studio ya Studio Harry Son. Ndani yake, amepata usaidizi mkubwa wa sauti za uitikiaji kutoka kwa wasanii wengine ikiwa ni pamoja na Niawou, Ballou Canta, Carlito, Djeffard Lukombo, Nyboma Mwa Dido na Shimita.