Chui milia
Chui milia | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chui milia wa Bengali
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nususpishi 5:
| ||||||||||||||||||
Msambao wa chui milia mnamo 1900 (machungwa) na wa kisasa (nyekundu)
|
Chui milia (pia: babara kutoka Kiarabu: babar; jina la kisayansi: Panthera tigris; kwa Kiingereza: tiger) ni mnyama mkubwa mlanyama wa familia ya Felidae katika ngeli ya mamalia, kwa hiyo chui milia hufanana na paka mkubwa.
Chui milia wanaishi katika Asia katika pembetatu kati ya Uhindi, Siberia ya kusini na Indonesia. Mazingira wanayoendelea ni misitu. Siku hizi idadi ya chui milia imepungua sana kutokana na upotevu wa maeneo na kuwindwa.
Chakula chao ni nyama inayopatikana kwa kuwinda wanyama wengine. Kama wanyama wengi wanaofanana na paka, chui milia hupendelea kuwinda peke yake. Kila mmoja ana eneo lake analoweka alama za mkojo na kulitetea dhidi ya chui milia wengine.
Ukubwa wa wanyama hao hutofautiana kutokana na maeneo yao na nususpishi zao. Wale wa Sumatra ni wadogo, wakiwa na urefu wa mwili (pamoja na kichwa bila mkia) sentimita 140 pekee na uzito wa kg 120. Mkubwa zaidi ni chui milia wa Siberia mwenye urefu unaopita mita 2 na uzito wa kilogramu 150 (jike) hadi 250 (dume). Aina ya Siberia ni kubwa kushinda simba wa Afrika.
Jike anazaa watoto 2-3 na kuwatunza kwa miaka 2 - 3. Baadaye wanapaswa kujitafutia eneo lao. Kwa umri wa miaka 3-4 anaweza kuzaa na kufikia umri wa miaka 20 - 25.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chui milia kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |