Nicolas Sarkozy
Nicolas Sarkozy (kwa jina kamili Nicolas Paul Stéphane Sarközy de Nagy-Bocsa; * 28 Januari 1955 Paris) ni mwanasiasa aliyekuwa Rais wa Ufaransa tangu 16 Mei 2007.
Sarkozy ni mtoto wa baba mkimbizi kutoka Hungaria na mama wa asili ya Kiyahudi. Alijiunga na siasa akawa mwenyekiti wa chama cha UMP cha rais Jacques Chirac akateuliwa kuwa mgombea wa chama hiki.
Chini ya rais Chirc akawa waziri wa mambo ya ndani kwa miaka mingi. Akajipatia sifa ya kuwa mkali dhidi ya wageni na wahamiaji waliovunja sheria akidai kuwarudisha katika nchi walipotoka au hata nchi za mababu.
Tangu kuwa rais alishangaza watazamiaji wengi kwa kuingiza mawaziri kutoka chama cha upinzani (parti socialiste) katika serikali yake pamoja na mawaziri wenye asili ya Kiafrika na Kiarabu kati yao Rachida Dati (waziri wa sheria), Fadela Amara (waziri msaidizi wa nyumba na maendeleo ya miji) na Rama Yade (waziri msaidizi wa mambo ya nje kwa haki za binadamu).
Mwezi wa Oktoba 2007 Sarkozy alitangaza talaka na mke wake Cécilia Sarkozy atakayeendelea kulea mtoto wao wa pamoja.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Nicolas Sarkozy Construire Ensemble—Official web site of the presidential campaign Ilihifadhiwa 7 Juni 2007 kwenye Wayback Machine.
- Website of the UMP, Sarkozy's party Ilihifadhiwa 21 Mei 2015 kwenye Wayback Machine.
- Nicolas Sarkozy Ilihifadhiwa 5 Machi 2021 kwenye Wayback Machine.–Official Website
- Supporters de Sarkozy–Official Website of Nicolas Sarkozy's supporters
Magazeti
[hariri | hariri chanzo]- Charlie Rose show 02.02.07 (video interview at Place Beauvau, Paris with PBS journalist Charlie Rose, 30.01.07)
- Sarkozy takes over Chirac's UMP party (BBC)
- Profile: Nicolas Sarkozy (BBC)
- Nicolas Sarkozy: French Choose the American Way? Ilihifadhiwa 4 Agosti 2016 kwenye Wayback Machine. by David Storobin
- Vive this difference Ilihifadhiwa 3 Mei 2012 kwenye Wayback Machine. by Suzanne Fields
- France's chance, Economist, 12 Aprili 2007
- Letter From Europe- Round 1 Jane Kramer, The New Yorker, 23 Aprili 2007