Asili ya Kiswahili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nadharia ya Kiswahili)

Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayotumiwa na watu katika mawasiliano hasa Afrika Mashariki na ya Kati.

Kama lugha nyingine zote, hii pia ni sauti za nasibu zenye mpangilio maalumu zilizokubaliwa na watu ili zitumike kwa mawasiliano.

Historia ya suala la chimbuko la lugha[hariri | hariri chanzo]

Chimbuko ni istilahi yenye maana ya kitu fulani kilipoanzia. Ni dhahiri kuwa kuna mijadala ya wataalamu mbalimbali inayozungumzia chimbuko la lugha ya Kiswahili.

Baadhi ya wataalamu hao ni pamoja na Chami (1994), Massamba na wenzake (1992 mpaka 1996), Freeman Granville (1959) na wengineo. Ifuatayo ni mitazamo yao kukusu chimbuko la lugha ya Kiswahili.

Chami (1994), Massamba na wenzake (1992 hadi (1996) wanasema utafiti uliofanywa na wataalamu wanaosema kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ni Kingozi kizungumzwacho Kenya na Kishomvu kizungumzwacho maeneo ya Bagamoyo na Dar es Salaam hauna mashiko, hivyo basi litakuwa ni jambo la busara kama watafanyia upya utafiti wao.

Nae Freeman Granville (1959) Katika kitabu chake alichokiita "The Medieval of Kiswahili Language" anasema Kilwa hata kabla ya karne ya 10 ilikuwa na umuhimu mkubwa kibiashara, hivyo basi kulingana na umuhimu huo wa kibiashara miongoni mwa Wabantu wa Kilwa na wageni (Waarabu) ilipelekea kuibuka kwa lugha moja ambayo ndiyo inasadikika ni Kiswahili cha leo.

Wapo wataalamu wengine wanaosema kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ni huko Afrika ya Magharibi (Kamerun). Wao wanaseme kuwa kwa kuwa Afrika ya Magharibi ndiko chimbuko la Wabantu wa mwanzo yawezekana ndiko Kiswahili kilipoanzia.

Pia wataalamu wengine wanasema chimbuko la lugha ya Kiswahili ni huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hawa wanasema baada ya wale Wabantu wa mwanzo kutoka Afrika Magharibi kukaa kwa muda mrefu katika misitu minene ya Kongo walianza kutawanyika kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kutafuta maeneo yenye uoto wa asili, hivyo walijikuta wakitokea kingo za Uganda na Kigoma hadi kufikia Ziwa Viktoria walikaa hapo kwa muda mrefu hadi walipoamua kuondoka maeneo hayo na kuelekea katika mabonde yenye rutuba ya mto Tana katika visiwa vya Shupate na Shungwaya.

Baadae mwaka 1999 Massamba na wenzake wakaja na kusema kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ni upwa wa pwani ya Afrika Mashariki. Wao wanamalizia kwa kusema kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ni matokeo ya muingiliano wa muda mrefu kati ya Wabantu waliokuwa wakizungumza lugha zao za asili (Kibantu). Hivyo basi ni ukweli kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ni pwani ya Afrika Mashariki.

Hivyo, kuhusu asili ya lugha hiyo kuna nadharia mbalimbali, kama vile:

Kiswahili ni Kikongo[hariri | hariri chanzo]

Nadharia hii inaeleza kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni huko nchini Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo). Inasemekana kwamba pwani ya Afrika ya Mashariki hapo mwanzo ilikuwa haikaliwi na watu, lakini kutokana na ugumu wa maisha hapo baadae watu kutoka maeneo ya Kongo walihamia pwani ya Afrika ya Mashariki. Watu hao bila shaka walihama na lugha zao ikiwemo Kiswahili.

Sababu hizo hazina mashiko kutokana na kuwa wanahistoria hawajaeleza ni lini hasa watu hao walihamia maeneo ya pwani ya Afrika ya Mashariki.

Kiswahili ni Pijini au Krioli[hariri | hariri chanzo]

Nadharia hii inasema kwamba wakati Waarabu walipokuja pwani ya Afrika ya Mashariki walioa wanawake wa Afrika na hivyo kutokana na mwingiliano wa lugha zao tofauti ilizaliwa lugha mpya ambayo ni aina ya Pijini.

Baadaye watoto walipozaliwa walikuta lugha hiyo mpya ambayo ni Pijini. Watoto hao waliiendeleza lugha waliyoikuta na baadaye ikazaliwa Krioli, yaani Pijini iliyokomaa.

Kiswahili ni Kibantu[hariri | hariri chanzo]

Wanahistoria wanaeleza kuwa Kiswahili kimetokana na Kibantu kwa kutoa sababu mbalimbali. Miongoni mwa sababu hizo ni:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asili ya Kiswahili kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.