Mwanaume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Michelangelo alichonga sanamu ya Daudi kama kielelezo wa maumbile ya mwanaume

Mwanaume (pia: mwanamume) ni binadamu wa kiume. Kwa kawaida ni mtu mzima anayeitwa hivi kwani wanaume wadogo huitwa watoto wa kiume tu au wavulana.

Wanaume ni takriban nusu ya binadamu, wengine huwa wanawake. Wanaume na wanawake ni jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.

Kuna tabia za pekee katika maumbile ya mwili. Wanaume huwa na viungo vya uzazi vya kiume ambavyo ni pekee kama vile mboo (uume, dhahakari) na pumbu (korodani). Wakati wa kubalehe homoni ya testosteroni inaongezeka mwilini mwa mwanaume na kusababisha tabia kama sauti ya chini, kongezeka ya nywele mwilini (kwa mfano ndevu), kuongezeka kwa upana wa mabega na kiwango cha musuli mwilini kulingana na wanawake. Msingi wa tofauti hizi ni hasa chembeuzi kinachoitwa "Y" yaani wanaume wana jozi la vyembeuzi "X" na "Y" ndani ya seli zao lakini wanawake wana jozi la "X" mbili. Chemebuzi ya Y inabeba habari zote zinazomfanya mwanadamu kukua kama mwanaume badala ya mwanamke.


Lakini si tofauti za mwilini pekee zinazosababisha wanaume kuwa tofauti na wanawake. Kuna pia tabia za kiakili na kiroho za pekee zinazoonekana kati ya wanaume wengi. Hata hivyo tofauti nyingi zinategemea pia utamaduni kwa sababu mara nyingi watu wamepanga shughuli na pia namna ya maisha tofauti kwa wanaume na wanawake na watu wamezoea kuchukua matokeo ya mapatano haya kama jambo la kimaumbile hata kama ni kiutamaduni tu.

Pamoja na hayo kuna wanaume wasio wachache sana wenye tabia zinazotazamiwa kuwa za kike kwa sababu miili yao huwa na viwango tofauti za homoni kama testosteroni na estrogeni. Kuna watu kadhaa wenye mwili wa kiume wanaojisikia kuwa wanawake.


People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanaume kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.