Musalia Mudavadi
'
Musalia Mudavadi | |
---|---|
Mudavadi alitumikia kama Waziri mkuu msaidizi nchini Kenya kuanzia Aprili 2008 mpaka Aprili 2013 | |
Amezaliwa | 12 Septemba 1960 |
Kazi yake | mwanasiasa maarufu nchini Kenya |
Wycliffe Musalia Mudavadi (anajulikana zaidi kwa jina la Musalia Mudavadi; alizaliwa katika Kaunti ya Vihiga, 12 Septemba 1960) ni mwanasiasa maarufu nchini Kenya.
Mudavadi amekuwa mbunge kwa miaka mingi. Aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1989 baada ya baba yake, Moses Mudavadi, aliyekuwa akishikilia kiti hicho, kufariki.
Alikuwa ndiye makamu wa rais wa mwisho kabla Daniel Arap Moi hajaondoka madarakani. Inaaminika kuwa alipewa umakamu wa rais ili kushawishi Waluhya kuiunga mkono KANU. Mpango huu haukufanikiwa.
Katika uchaguzi wa urais nchini Kenya mwaka 2002, Mudavadi alikuwa mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta. Pamoja na kuungwa mkono na rais aliyekuwa akimaliza muda wake, Moi, na mtandao mkubwa wa KANU, Kenyatta na Mudavadi walishindwa uchaguzi, Kenyatta hakuchaguliwa kuwa rais na Mudavadi alipoteza kiti cha ubunge wa Sabatia.
Wakati wa upigaji wa kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Kenya, Mudavadi alikuwa kwenye kambi iliyokuwa ikiipinga katiba hiyo. Katika kambi hiyo alikuwemo mwanasiasa maarufu Raila Odinga.
Mudavadi alikuwa kwenye kambi ya watakaogombea urais wa Kenya mnamo Desemba 2007. [1]
Mwaka 2015 alianzisha chama cha Amani National Congress (ANC)[2][3] kilichoendelea kusimama upande wa Raila Odinga kwenye uchaguzi wa rais mnamo 2017.[4]
Mwaka 2021 Mudavadi aliungana na Kalonzo Musyoka (chama cha Wiper), Moses Wetangula (Ford Kenya) na Gideon Moi (Kanu) kuunda ONE KENYA ALLIANCE-OKA kwa kusudi la kumpata mgombea kwenye uchaguzi wa 2022. Mudavadi alitangaza kwamba yeye alilenga kugombea mwenyewe[5].
Tarehe 23 Januari 2022 Mudavadi alimkaribisha makamu wa rais William Ruto kwenye mkutano mkuu wa ANC na hivyo kusababisha wenzake Gideon Moi na Kalonzo Musyoka kuondoka kwenye ushirikiano naye.[6]
Marejeo
- ↑ Tovuti Ilihifadhiwa 18 Desemba 2021 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Amani National Congress my new vehicle, says Mudavadi Daily Nation, 3 May 2015
- ↑ Amani lists first members Daily Nation, 27 June 2015
- ↑ Mudavadi heads back home to plot ANC’s next big move Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2017 kwenye Wayback Machine. The Star, 25 October 2017
- ↑ I want to reclaim the soul of Kenya, Musalia Mudavadi, The Standard 23.02.2022
- ↑ Kalonzo, Gideon: Why we walked out of Musalia Mudavadi's ANC’s event, The Standard 23.01.2022
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Musalia Mudavadi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |