Mtumiaji:Muddyb/Hip hop ya Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hip-hop ya 'Tanzania, japo huwekwa katika kundi la Bongo Flava. Hii inatokana na mchanganyiko au elementi za pop na midundo ya Kitanzania. Kumekuwa na midahalo kadha wa kadha juu ya Bongo Flava, ambayo imejiibua ikiwa kama miondoko ya pop, ya kwamba inastahili kutumia istilahi ya "hip hop" na si jina la kipekee ambalo halihusiani kabisa na elementi za hip hop,[1] huku ikiwa inaendelea kujijenga katika misingi tofauti kabisa na hrdcore rap au, kwa mfano, kundi la Hip-hop la X Plastaz, ambao wao wanatumia muziki wa kimila ya Kimasai kuundia muziki na staili yao kwa ujumla.[2] Hip hop ya Tanzania ilianza katika miaka ya 1980 wakati huo vijana wa Kitanzania walikuwa na mapenzi ya juu na muziki wa hip hop wa Marekani. Hapo awali, walichukua biti za rap na hip hop za Kimarekani na kuimbia juu yake. Wakati vijana wakirap, polepole ikaanza kujitengeneza katika maudhui ya muziki wa asili ya Kitanzania kwa kuunda muziki wa aina yake yenyewe. Matokeo yake, ikaanza kuonesha shauku kutoka kwa vijana wengine kutoka katika maeneo ya Afrika Mashariki.[3]

Staili ya muziki wa Bongo Flava[hariri | hariri chanzo]

Bongo Flava ni muziki wenye wendo kasi na huimbwa kwa Kiswahili. Jina la “Bongo Flava” linatoka na jina la utani la Dar es Salaam. Ina maana ya kwamba unahitaji akili ili uweze kuishi katika jiji hilo. Ina husisha elementi mbalimbali ili kujenga muziki huu, hasa rap ya Kimarekani, R&B, hip hop, ikiwa na twisti kali la Kiswahili ndani yake. Kama jinsi ilivyo tamaduni za muziki wa hip hop wa Kimarekani nazo zimo vilevile katika mashairi ya hip hop ya Tanzania yenye kuhusu, UKIMWI, umaskini na rushwa, au kuhusu maisha, mahusiano, fedha, wivu na mapenzi.[4]

Bongo Flava ni mseto wa Afrobeat na melodi za Kiarabu, dancehall na midundo ya hip-hop, na mashairi ya Kiswahili.[5] Muziki huu ulianza kujengwa katika miaka ya 1980 wakati vijana wa Kitanzania walipoanza kuvutiwa kuimba muziki wa hip hop wa Marekani.Haraka wakaongeza ladha zao katika muziki huo na kutengeneza midundo yenye mahadhi ya kinyumbani, mizani, na hoja zake pia. Aina hii ya muziki imekuwa maarufu kwa haraka sana; umekuwa miongoni mwa muziki unaouza vizuri katika Afrika ya Mashariki, na tayari ushapata mafaniko katika nchi za jirani kama vile Kenya na Uganda, na kusambaa maeneo mengine ya Afrika na duniani kwa ujumla. Mwaka wa 2004, studio ya Kijerumani Out Here Records ilitoa kompilesheni ya CD ya Bongo Flava iliyoitwa Swahili Rap from Tanzania.[6] CD hiyo yenye dakika 70 ambayo ndani yake kuna wasanii kama X Plastaz, Juma Nature, na Gangwe Mobb wamefurahia usambazaji huo wa kimataifa.

Wakati hip hop ya Marekani inaingia Tanzania kwa mara ya kwanza, marapa wa ndani walichukua sampuli ya midundo ya rap ya Kimarenai, na kutia maneno ya Kiswahili katika neno la Kiingereza. Bongo Flava hiyo changa na kuiingiza hip hop kutoka Marekani awali ilikumbatiwa sana na watoto wa kishua ambao waliona kama fasheni kuiga miyenendo ya Kimarekani.[7] Hili lilitazamiwa kama kuiga tamaduni na mitindo ya Kimarekani kwa wakati ule. Hasa walionekana kama wapenda Umarekani. Mwanzoni mwa miaka ya 1990, wakati mtindo huu unakua kwa kasi, karibia kila rapa na wafokaji walianza kuvutiwa kuimba rap hizi kwa Kiswahili. Maamuzi hayo yalipelekea muziki huo kuvutiwa na vijana wa ndani sasa hasa kwa kufuatia lugha ya Kiswahili ndiyo lugha ya taifa na ndiyo lugha ya mazungumzo kwa kila raia wa Tanzania.[8] Kwa kuongezea, midundo ilihama kutoka ile midundo yenye mahadhi ya Kimarekani na kuanza kutengeza mizani, sauti na midundo ya kinyumbani zaidi. [7] Wasanii wa Tanzania walihakikisha wanarap kwa Kiingereza, lakini watadumisha Uswahili wao katika mashairi. Kuimba kwa Kiswahili, waliweza kutunga hip hop yenye muundo wa Kiswahili huku wakidumisha hali halisi ya hip hop ya Marekani.[9] Rap hii ya Kiswahili iliendelea kutumia fasihi na mila za Kiswahili kwa kuchezea maneno na mizani ili kujieleza. Hapo awali wasaniii wengi sana walijibidisha kutumia mawazo au fikra na tamaduni za Kiswahili katika nyimbo zao kuliko kuandaa upya pop na tamaduni za Rap za Kigansta za Kimarekani.[8]

Uamuzi wa matumizi ya lugha umechukua nafasi nzuri katika kukuza na kukubalika kwa muziki wa Bongo Flava nchini. Ingawa kurap kwa Kiswahili kwa wasanii wengi wapya waliweza kuswahilisha hip hop ya Marekani hasa katika nyanja za kisiasa na kuihusisha na tamaduni za ndani katika Tanzania. Rapa wa Kitanzaniar Dolasoul (Ahmed Dola), ambaye alisoma nchini Nigeria na Uingereza, alieleza ya kwamba muziki wa rap, hasa kwa Kiswahili, umemletea maana ya kuwawakilisha watu wake na kuongelea mabadiliko ambayo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kesho iliyo-bora’"[10] Pia ameeleza ya kwamba albamu zilitotayarishwa kwa Kiswahili na matumizi machache ya Kiingereza, inasaidia kufanya lugha yake kukubalika zaidi kimataifa. Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika bongo flava hufikisha ujumbe na azimio kwa wasikilizaji wake, inatia hamasa ya kujivunia utaifa na tamaduni kwa ujumla. Dolasoul anasema ya kwamba matumizi ya Kiswahili na Kiingereza kiasi katika nyimbo zake, anajaribu “kuwaamsha watu wake.” Wakati huohuo, muziki wa Rap wa Kiswahili unajaribu kuwakilisha maudhui yaleyale ya rap za nje lakini katika mtindo wa Kitanzania zaidi. Katika harakati za kuchukua mifano ya marapa maarufu wa Marekani ili kutengeneza muziki wa ndani, hili limepelekea kuonekana Tanzania kama vile inagezea muziki wa nje na sehemu kubwa walionwa kama wahuni tu. Kweli kabisa hao wanaogezea rap ya kihuni ya Kimagharibi walichukuliwa kama magangsta uchwara.[11] Hivyo basi matumizi ya Kiswahili katika Rap ya Tanzania imesaidia kuazimisha maudhui ya tamaduni ya Kiafrika zaidi. Hoja zilizokuwa zinaimbwa sana ilikuwa suala la kuweka usawa kwa wanawake, ambapo kwa kipindi hiko ilikuwa imeshika hatamu kuliko yale mashairi makali. Pamoja na yote, mitindo ya kushangaza ambayo inaonekana kushika hatamu au hupendwa na vijana wengi wa Tanzania, kwa mfano uimbaji wa kundi la LWP Majitu, kulingana na Out Here Records, LWP ni "moja kati ya makundi maarufu kwa mtindo wa mashairi ya kutisha"[12] Aidha katika maeneo maskini ya Tanzania au yale yenye maisha mazuri, ni vigumu sana wasaniii wa rap kuweza kudumisha mila na asili, si tu nchini hata huko ulimwenguni.

Kuibuka kwa hip-hop nchini Tanzania[hariri | hariri chanzo]

Kutoka kushoto: Samia X, Cool Moe Cee, Ibony Moalim na marehemu Kim.

Utamaduni wa hip hop nchini Tanzania ulianza mwanzoni na katikati mwa miaka ya 1980 hasa ikiwa kama harakati changa. Wakati huo mapromota na wasanii walilazimika kurekodi na kunakili muziki studio kwa zamu huku wakitumia vifaa hafifu kabisa. Rap ya awali. Haijaanza katika maeneo ya watu wenye hali ya chini ya kimaisha jijini Dar es Salaam, bali katika maenoe ambayo tayari yana athira ya muziki huo hasa mijini, ambapo vijana wengi walikuwa na fursa a u uwezo wa kupata vitu na nyimbo za dunia ya Kimagharibi kupitia marafiki, familia, na nafasi za kusafiri. Cha kushangaza, muziki wa rap ulikuwa unabamba zaidi kwa watu wa hali ya wastani. Hawa walikuwa vijana wenye elimu ya kawaida, wanaojua Kiingereza na uhusiano na watu wa nchi za nje ambao wangeliweza kuwatumia kanda au CD muziki kutoka kwao. Muziki wa hip hop umetoa chanzo kizuri kwa vijana wa Kitanzania kuelezea yale ya moyoni yanayoikumba jamii yao.[13] Wanafunzi hawa wa hip hop wamecheza nafasi kubwa katika uanzishwaji wa bongo flava, "hasa kwa kupitia ushiriki wa tamaduni mbalimbali za ndani ya nchi, malugha na bila kubaguana rangi na kuifanya hip hop ya nchini iwe ya kimataifa, hasa kwa kuunganisha lugha ya Wamarekani Weusi na kutia maneno ya Kiswahili na maneno ya mtaani ("Kihuni")".[14] Katika miaka ya 1990, hip hop ya Tanzania ilhama kutoka katika misingi ya kuimba kwa kujifurahisha na kwenda kuwa muziki unaokubalika kibiashara, hii ilipelekea upate kujulikana na vijana wengine wa hali ya chini.

Conway Francis akiwa na mpenzi wake, Johanna huko Ilala katika miaka ya 1990. Conway alikuwa mwanachama wa kundi la "Three Power Crew" ambalo ndani yake alikuwa anakuja Fresh XE, Young Millionaire na Con mwenyewe. Con alikuwa machachari sana.

Rap ya awali ya Tanzanian ilikuwa kwa Kiingereza tu, lakini wakati mtindo huu unakua baadhi ya marapa wakaanza kuandika mashairi yao kwa Kiswahilii. Shindano la kwanza la muziki wa rap nchini Tanzania lilianzishwa na marehemu Shaban Sato mnamo 1989/90 katika ukumbi wa Lang’ata. Kupitia mashindano haya, ndipo marehemu Kim and the Boyz (Abdulhakheem Magomero) na Ibony Moalim walipopata wazo la kuanzisha mashindano makubwa ya rap maarufu kama Yo Rap Bonanza katika ukumbi uleule wa Lang’ata Kinondoni..[15] Emsii usiku huo alikuwa DJ Junior Challenger almaarufu Amani Misana (Mzee wa Pillow Talk). Usiku wa shindano uliambatana na kudansi (wakati huo waliita B Boying) akina Othman Digadiga, Sammy Cool na Bob Rich, Mzee Bachu, Ommy Sidney, Black Moses , Maganga, Hafidh, Ali Baucha wengine wengi walionesha uwezo mkali wa "Break Dancing". Kwa upande Ma-emsii walikuwa wengi sana ikiwa ni pamoja na Coneway Francis (wakati huo alionekana kuwa tishio katika rap na alivutia wengi kuingia katika shindano). Inasemekana Conway alikuwa na suati zito ambalo lililkuwa kivutio wakati huo na aliimba na dada mmoja aliyefahamika kama Janeth (Janet Jackson). Ma-emsii wengine ni pamoja na DJ Young Milionea, DJ.Danny Star, Mukama Muganda GTRM, KG 40 (Kelvin Ndunguru) na kundi lao la the Raports akiwa na wakina G Pupple(George Kusila) KBC (Kibacha) na Makili, Chief Rymson na kundi zima la Villian Gangster (baadaye ikaungana na kundi lingine la rap na kuunda Kwanza Unit), Eddy Cox, Dika Sharp, Fanani (Trigga F) na Ibony Moalim (ambaye wakati huu alikuwa ana floo na kurap), na wengine wengi. Katika usiku huu, Coneway Francis alitisha kupita maelezo. DJ Danny Star (aliiimba Summer Holiday Rap) KG 40 na Fresh XE ambaye kwa nyimbo hiyo hiyo ya “Piga Makofi Tafadhali ndiye aliyeibuka mshindi wa taji la Rap. Kwa bahati mbaya kukatokea vurugu, hasa kutoka kwa vijana wa Illaa na watu wengine wanaompenda Coneway Francis wakafanya fujo na kudai kuwa ushindi uende kwa Coneway hata hivyo matokeo hayakuweza kubadilishwa.

Shindano la pili la Yo! Rap Bonanza, ambalo lilifanyika katika ghorofa ya saba katika hoteli ya New Africa. Safari hii, makundi ya rap yaliongezeka mno kupita wale wa kwanza. Hii sasa ilivutia hata watu kutoka nje ya Dar es Salaam, na ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Saleh Jabry kushiriki katika mashindano ya Yo Raps. Upande wa majaji alikuwepo Ibony Moalim - kama Chief Jaji, DJ Saydow, Mark (Mzungu wa Holiday Hotel),na Slim (Check Bob Maarifa). Upande wa wasanii walioshiriki ni pamoja na Kool Moe Cee, Kool X, MGM, Tough Jam, Big Money, DJ Edy Cox, Nigga One (Adili Kumbuka) na kundi zima la Raiders Posse, Chief Rymsom, Lady Tassy, Killa B, Easy B na kundi lao la the Bad Mother's, KG 40 (Kelvin Ndunguru), KBC (Kibacha), Saleh Jabry, P Funk na kundi lake la No Name, Mukamuganda GTRM, Mahadia Kumbuka. Upande muongozaji wa tamasha alikuwa DJ. Rusual na lugha iliyotumika ilikuwa Kiingereza. Rusual (wa Jetset Discotheque - Msasani Beach) ndiye aliyendeshsha shindano, aliweza kurap kidogo kwa Kiswahili na hata alitia na Kidigo kuboresha na watu walipenda sana. Wakati shindano linaendelea, mmoja kati ya majaji usiku huu uzalendo ulimshinda na kuanza kuingia stejini na kuanza kuruka majoka wakati zamu ya Saleh Jabry (jaji mwenyewe alikuwa Slim - Check Bob Maarifa). Alifanya hivyo kila alipokuwa anaingia Saleh Jabry. Suala hili lilipelekea shindano hilo kusimama kwa muda hadi hapo walipopatana na majaji wenzie asifanye hivyo. Zogo lilikuwa kubwa, lakini hatimaye waliyamaliza kikubwa. Mtindo aliokuwa nao Saleh Jabry ni ule wa kuchanganya maneno ya msimu ya Kiingereza na Kiswahili kidogo. Inasemekana katika usiku huo, ni watu wawili tu ndio waliongea Kiswahili, DJ Rusual na Saleh Jabry tu, lakini wengine wote walikuwa wanamwaga Kiingereza tu (hii ikiwa kama mwigo wa mtindo halisi wa rap ya Kimarekani). Hata matusi aliyokuwa anatukanwa Slim yalikuwa kwa maneno ya msimu ya Kiingereza cha Kimarekani. Pamoja na kushiriki wasanii wengi na mazogo ya hapa na pale, mshindi wa usiku huo akawa Saleh Jabry. Tamasha/shindano hili la Yo Raps ! Bonanza ilifanyika Mara sita. Tamasha hili lilileta hamasa kwa watu wengi baadaye. Miongoni mwao akina Issa Michuzi waliokuwa tayari kutoa taarifia hizi katika magazeti nchini. Akina DJ Jummane (Mzungu Mholanzi maarufu DJ J4 au Jumanne Thomas). DJ huyu ambaye baadaye kaja kuwa kama mwanaharakati halisi wa muziki wa hip hop ya Tanzania. Kaenda mbali zaidi kwa kuwa kama meneja wa kundi zima la Xplastaz na mwaka wa 1997 akaanzisha wavuti ya Rhumba Kali (baadaye na hadi sasa inaitwa “African Hip Hop.com). DJ J4 ana nafasi kubwa katika muziki wa hip hop ya Tanzania, kwanza akiwa kama mshabiki nambari moja kutoka nchi za nje, na mtunza kumbukumbu mkuu wa muziki huu wa hip hop ya TZ.[16]

Hakuna siri ni kweli kwamba, muziki wa Wamarekani Weusi ndio hasa ulioleta athira ya kurap kwa vijana wa Tanzania, hasa ule muziki wa soul na R&B, lakini kutokana na muundo wa serikali ya kisoshalisti kwa kipindi hicho, muziki wa nje ulipigwa marufuku nchini Tanzania. Kwa mfano kundi la hip hop la wakati huo Tanzania liliitwa Berry White, liliiga vilevile muziki wa Marekani na kwenda miyenendo ya upigaji uleule wa kama Barry White mwenyewe wa mamtoni. Isitoshe, kabla ya serikali ya kisoshalisti kuzuia muziki wa nje usiingie nchini Tanzania, dhahiri hip hop ya Tanzania ilikuwa ishaathiriwa na muziki wa majuu, hasa ule wa Wamarekani Weusi.[17] Hili nalo lilikianza fursa kwa vijana wa Tanzanian kujua hip-hop, na hata hao wasanii wa awali aidha walijifunza kwa kusikia kupitia nchi za nje au wapate mawasiliano kutoka ughaibuni.[18] Kwa baadhi ya waghani vijana kama Dolasoul, au Balozi, (Ahmed Dola), "walifanya rap kwa kujifurahisha tu, pesa haijahusika." Muziki wa rap ulikuwa sehemu ya burudani ya kupotezea muda uende kwa watoto wa kishua, hii ni tofauti kabisa kwa wasanii wa awali wa Marekani na Afrika Kusini. Elimu walitumia kama msingi wao wa kujipatia mafanikio katika jamii na hao waghani wa awali walighani (rap) kwa kutumia mashairi ya nyimbo za Wamarekani Weusi.[4] Kibao kilianza kubadilika mwanzoni mwa miaka ya 1990 wakati wa kuvunja sera ya ujamaa, suala hili lilitoa fursa kwa ngoma za hip-hop kuweza kusikilizwa hata na wale watu wa hali ya chini na kuongeza mzunguko, na hapa ikakubalika na wasanii wa ndani na wapenzi wakapatikana na rekodi zikaanza kufanywa, unakili na usambazaji wa hip-hop.[19]

Afrika katika kuchukua aina hii ya muziki, katika historia ya muziki wa hip hop Tanzania, haijapato kutokea msanii wa kiume wa hip hop kupata kuchaguliwa katika tuzo za muziki za Kora Afrika hadi hadi mwaka 2005 msanii Ambwene Yesaya aka AY alipotajwa katika moja ya kategoria katika tuzo hizo ya Msanii Bora wa Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka wa 2005.[20] Kwa tuzo hizi inaonesha kiasi gani muziki huu umesogoea ndani ya muda mfupi.

Kwa sasa, hip-hop si muziki wa watu wenye uwezo tu, bali pia umekuwa kama chombo muhimu cha kupazia sauti hata za wale wanyonge. Kwa kutumia hip hop, wenye hali duni wanaweza kuelezea hisia zao kuhusu yale yanayoendelea nchini. Vilevile ilitumika kama njia ya kutia hamasa vijana waweze kujiongezea kipato. Katika hali yoyote ile, wale wenye hali duni hutumia hip hop kuelezea hisia zao na wakati huohuo wanaitumia kama chanzo cha kujikwamua kiuchumi.

Kwa mujibu wa mwanahabari Henry Bukuru (a.k.a. Cxteno Allstar), mzuki wa rap ulikuwa hasa ndiyo uliyoleta athira ya utamaduni wa hip hop nchini Tanzania. Mponjika aliwahi kuelezea elementi nne za utamaduni wa nchini Tanzania: break dancing (b-boying), graffiti, DJing, na rapping. Mashindano ya UDJ yameleta kuzaliwa kwa hip hop, hasa huko Zanzibar, ambapo kulikuwa na televisheni inarusha mashindano haya yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja visivyo rasmi kwa ajili ya mashindano hayo (mahafali ya shuleni, pikiniki, majumba ya sherehe).[4][21]

Miongoni mwa wasanii waliosukuma muziki wa hip hop nchini Tanzania ni Mr. II. Mr. II huweka katika kundi la wasanii wanojitegemea, lakini kuna wakati muziki ulikuwa unatamba kikanda na makundi mawili yalishika chati kupita maelezo. Makundi ni pamoja na "TMK" na "East Coast". Wasanii wanaotokea TMK ni pamoja na Juma Nature au Gangwe Mobb.[22] Kwa upande wa kina "East Coast" ni wale waghani ambao hujiweka katika daraja la juu na hutokea huko Upanga, wachanaji hawa hurap kuhusu maisha na starehe za maisha, hasa muziki wa kibiashara tu. Wakati wasanii kutoka TMK mfano akina Juma Nature wanarap kuhusu mambo ya nchi na mshikamano. [23]

[24]

Wasanii wa awali wa rap ya Tanzania[hariri | hariri chanzo]

Adili Kumbuka, lakabu Nigga One. Alikuwa mchanaji maarufu sana kwa watoto Ilala. Katika shindao la Yo Rap Bonanza la mwaka 1992, Nigga One alichukua nafasi ya pili, na ya kwanza ikaenda kwa Saleh Jabri. Kundi lake lilikuwa Raiders Posse kabla kuundwa KU Crew. Alikuwemo KBC, D-Rob, Eddy Cox, James Paul Wamba na wengine wengi.

Sehemu kubwa ya hip hop ya Tanzania ilianza na watu ambao siku hizi hawatajwi kabisa au mchango wao unaonekana hafifu. Baadhi ya wasanii walioanzisha hasa gurudumu la muziki wa hip ho ya Tanzania.

Kifupi, hip hop ya Tanzania, sehemu kubwa ya wasanii walianza kwenye miaka ya 1985 hadi 1987. Zama hizi kulikuwa na mashindano ya kurap katika maeneo mbalimbali hasa majumba ya starehe na masheleni. Ukikutana na mtu anayeweza kuchana kwa Kiingereza lazima ushindane nae mtu kwa mtu hadi kieleweke. Wakati Saleh Jabri alivyojitafsiria wimbo wa Ice Ice na kurekodi mwishoni mwa mwaka 1991, wimbo haukupendwa sana na marapa wa Tanzania bara kwa sababu wakati huo watu kitambo walishaanza kuchana katika kumbi mbalimbali jijini Dar kama vile Twiga, New Chox, Coco Beach na nyingine kibao tangu 1987. Pamoja na yote, bado hakukuwa na rekodi rasmi zilizotolewa.

Kwa vile walifanya kwa kujifurahisha, watu walikuwa wanakutana chini ya uangalizi wa Bonny Luv, na makundi yakaanza kuundwa kwa kasi ya ajabu kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1993. Hata rekodi za awali ilianza tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990, lakini sehemu kubwa ya nyimbo hizo ilikuwa kwa Kiingereza japokuwa kulikuwa na baadhi ya wasanii waliokuwa wanakinukisha kwa Kiswahili japo si sana.

Kwa kipindi kile ilikuwa aidha uende kwa watayarishaji huko Masaki au studio za Clouds na rap ilikuwa inakua kwa kasi. Nilipewa upendeleo wa kipekee kwa kudondosha wimbo wa "Oya Msela"' na Clouds Ent 1991 lakini sikuwa wa kwanza kuimba kwa Kiswahili, kulikuwa na wajuvi zaidi yangu kabla ya mimi. Lakini umaarufu wa wimbo ulishika hatamu na kupigwa sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama vile ITV ulitazamiwa kama wimbo wa kwanza wa rap wa video kurushwa katika runinga hiyo. Kwa hakika ilimaliza nyimbo za rap ya Kiingereza kwa sababu tangu hapo wengi walitamani nao kuimba kwa Kiswahili. Baada ya kibao hiki, nilipata simu kutoka kwa Mr II lakabu Sugu akisema, ahsante kwa kufunifungua macho.

Huko nyuma kulikuwa na mgomvi mengi yasomana lakini tuliyamaliza vyema kabisa. Sipendi kuyaelezea sana kwa sababu pale uvutio unapokutana na sanaa, ubunifu huwa kileleni.

Salaam kwa wale wote walioshika maiki miaka ya nyuma hata kama ilikuwa japo kwa dakika tatu.

Sindila Assey mnamo 8 Mei, 2017

*Fresh X E - jina halisi ni Edward Mtui na ndiye hasa mwanzilishi wa kurap kwa Kiswahili katika miaka ya 1980 na alikuwa akiimba wimbo wake kwa kiitikio cha "Piga Makofi" ambao aliubadilisha wa Run-D.M.C. Clap Your Hands, lakini hajaurekodi. Kwa kuenzi uwepo wa Fresh na mchango wake katika tasnia, Professor Jay akatengeneza wimbo wa Piga Makofi kwa kutumia kiitikio kilekile cha Fresh kisha kutaja hazina kubwa ya wasaniii walioanzisha hip hop ya Tanzania.

*Young Millionaire

*Conway Francis

*Mawingu Band lakabu the Clouds - ilikuwa bendi iliyotamba na wimbo wa "Oya Msela" wimbo ambao unatoka katika albamu yao ya mwaka wa 1994, Msela.

*Cool James lakabu Mtoto wa Dandu

*Adili Kumbuka lakabu Nigga One - alikuwa mmoja kati ya wasanii mahairi sana katika rap ya Tanzania. Vilevile alishiriki vilivyo katika kuanzishwa kwa Kwanza Unit mwanzoni mwa miaka ya 1990 bahati mbaya hakuona matunda yake kwani alikuja kufa katika ajali ya gari mnamo mwaka wa 1993. Kulingana na duru, Nigga One inasemakana alikuwa hatari sana kwa kufoka. Wasanii wengi walimhofia kupambana nae katika mashindano ya rap. Sindila anamwelezea Nigga One

To be honest, a lot of icons where with Kwanza Unit, One, Ramzy, KBC, Easy B just to name a few. One aka Adili was the most stubborn influence behind every stage. He never shy away from an empty instrumental. He will annoy any DJ to get the piece of his lyrics out anytime anywhere. A very humble dude he was. He would always share a stage with his crew (KU) and anyone who's willing to try him. That's the interview you would have loved to have. I instantly became a friend when KBC introduced me to all (KU)one afternoon day at Twiga when DJ Bonny Luv asked of me. I was nervous, KBC was telling them I can do Treach all day... my gf was there too. In front of KU I did prove myself. Adili was jumping up n down. We then set for a New Chox cinema show. 'One' was unique on the microphone. He flowed like The late Guru and would get on any track.

Sindilla Assey

*Kwanza Unit - miongoni mwa makundi ya kwanza kabisa katika hip hop ya Tanzania. Kiufupi, KU ndiyo kundi la kwanza kuundwa katika tasinia nzima ya muziki wa hip hop ya Tanzania. Kuundwa kwa kundi ni juhudi kubwa na za dhati kutoka kwa Zavara Mponjika na hayati Nigga One. Kabla ya muungano, kulikuwa na mabifu kibao yasomana na ilibidi waungane li kuondoa mabifu na kukuza muziki kwenda kiwango kingine. Kuungana kwao, kulifanikisha mambo mengi kama wasanii waasisi wa rap ya Tanzania.

*Hard Blasters - kundi ambalo hutazamiwa kuleta mabadiliko katika muziki wa hip hop ya Tanzania

*Da Young Mob - kundi ambalo II Proud alipanda nalo katika kinyang'anyiro cha Yo Rap Bonanza, 1993

*Deplowmatz - Wakati wanaanza harakati ilibidi kwanza wamuone Sindilla kwa ushauri zaidi. Muda mfupi baadaye wakarekodi nyimbo zao mbili za kwanza "Turuke kwa Furaha" na "Word is Born".

*Wagumu Weusi Asilia lakabu W.W.A

*Black Houndz

*Bantu Pound

*Niggaz with Power (NWP)

*Full Soldiers 

*Rough Niggaz 

*Kibo Flava

*The Mac Mooger

*Mabaga Fresh

*KNT Squad 

*Ras Pompidue

*Saleh Jabir - msanii wa kwanza wa hip hop ya Tanzania kurekodi na kusambaza kazi zake. Japo mwenyewe hakuonesha kutaka kusambaza kazi zile bali alikuta tayari mzigo uko sokoni na baadaye kukamia ili apate chochote kitu. Inaaminika ndiye hasa aliyeanzisha kurap kwa Kiswahili, hasa kwa kufuatia shindano la Yo Rap Bonanza la mwaka 1992 na kuibuka mshindi. Saleh Jabri hutazamika kama ndiye chachu aliyesabisha wasanii wengine wa muziki wa hip hop ya Tanzania kuuanza kuimba kwa Kiswahili. Kabla ya Saleh J kushiriki kwenye tamasha la Yo Rap Bonanza, lugha kuu ilikuwa Kiingereza, lakini Saleh alitumia Kiswahili katika tungo zake. Hasa alifanya kunakili nyimbo za Kimarekani, kama vile Ice Ice Baby ya Vanilla Ice na kuimba kwa Kiswahili.

*Sos B

*Niggaz 2 Public

*Xplastaz 

*Underground Souls

*Ugly Faces - Hawa walikuwa wasela waliotambushwa wa Sindila Assey wa Mawingu Band na walifanya balaa zito kaktika mazoezi yao. Ndani yake anakuna Mac D, DJ Rich Maka na Eazy Daz. Kwa pamoja wakafanya ngoma moja na Bonny Luv iliyokwenda kwa jina la "Wapambe Nuksi" mnamo mwaka 1997.

*Big Dogg Pose

*GWM

*L.W.P

*Afro Reign 

*Pyscho Tak 

*2Proud 

*No name - kundi ambalo P Funk alikuwa mwanachama wao na Mchizi Karabani.

*King Crazy GK

*Gangwe Mobb

*Hashim Dogo

*Bugsy Malone

*Kool X

*Cool Moe Cee 

*Big Money

*4 Krewz Flava - miaka ya 1990 walihesabiwa kama akina Boyz II Men ya Tanzania. Lilikuwa kundi la mwanzo kabisa nchini Tanzania kuimba muziki wa R&B.

*Da Unique Sisters

*E Attack

*Juma Nature 

*Hardcore Unit

*Imeditation Kingdom

*Fun with Sense 

*Solo thang 

*Mack Malik aka Mac 2 B

Wasanii hao walishiriki vilivyo katika kuunda muziki wa hip hop nchini Tanzania

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Thomas, A. "X Plastaz & Bongo Flava: Tanzanian hip hop released internationally". africanhiphop.com. 
  2. Martin, Lydia. "Bongo Flava: Swahili Rap from Tanzania." afropop.org
  3. Mueller, Gavin. "Bongoflava: The Primer." Stylus Magazine, 12 May 2005
  4. 4.0 4.1 4.2 Lemelle, Sidney J. “‘Ni wapi Tunakwenda’: Hip Hop Culture and the Children of Arusha.” In The Vinyl Ain’t Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
  5. "Bongoflava: The Primer - Pop Playground - Stylus Magazine". 
  6. "Out - here records -". 
  7. 7.0 7.1 "Tanzanian Affairs » BONGO FLAVA". 
  8. 8.0 8.1 Lemelle, Sidney J. “‘Ni wapi Tunakwenda’: Hip Hop Culture and the Children of Arusha.” In The Vinyl Ain’t Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Press.
  9. The Language of the Young People: Rap, Urban Culture and Protest in Tanzania. Journal of Asian and African studies [0021-9096] Casco yr:2006 vol:41 iss:3 pg:229
  10. "Language choice and hip hop in Tanzania and Malawi | Popular Music and Society".  [dead link]
  11. Lemelle, Sidney J. “‘Ni wapi Tunakwenda’: Hip Hop Culture and the Children of Arusha.” In The Vinyl Ain’t Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 240. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
  12. "Bongo Flava". Out Here Records. 15 November 2004. Iliwekwa mnamo 6 March 2008.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  13. Lemelle, Sidney J. “‘Ni wapi Tunakwenda’: Hip Hop Culture and the Children of Arusha.” From The Vinyl Ain’t Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, 230-54. Ann Arbor, MI: Pluto Press
  14. How hip-hop culture is changing the wor(l)d - UCLA Today Online
  15. "Africanhiphop.com - the foundation of African hip hop online". 
  16. :: Historia fupi kuhusu muziki wa kizazi kipya wa Tanzania - African Hip-Hop Forum
  17. SwahiliRemix.com :: Tanzania Urban Culture Online - Mp3 Player
  18. "African Hip Hop in Tanzania- Highlights of a Conversation with Alex Perullo". Iliwekwa mnamo 2008-03-05. 
  19. Alex Perullo. "Bongo Flava". Iliwekwa mnamo 2008-03-05. 
  20. "kongoi.com". 
  21. "EastAfricanTube - East African Social Networking & Major Gateway in Media Sharing". 
  22. Bongo Flava (Still) Hidden „Underground”1 Rap from Morogoro Tanazania, Birgit Englert. URL:www.univie.ac.at/ecco/stichproben/Nr5_Englert.pdf
  23. http://www.afropop.org/explore/album_review/ID/2604/Bongo+Flava:+Swahili+Rap+from+Tanzania
  24. "Interview with Alex Perullo, by Banning Eyre and Sean Barlow - African Hip Hop in Tanzania – Highlights of a Conversation with Alex Perullo". 2005. Iliwekwa mnamo March 5, 2008.  Check date values in: |accessdate= (help)

External links[hariri | hariri chanzo]