Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Kati (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikoa ya Kenya
Mkoa wa Kati
Central Province
Mahali pa Mkoa wa Kati
Makao Makuu Nyeri
’‘‘Mji Mkubwa’’’ Nyeri
Eneo

- Jumla
Nafasi ya 5 kati ya mikoa ya Kenya
13,191 km²
Wakazi


 - Jumla (2007)  - Msongamano wa watu / km²
Nafasi ya 4 kati ya mikoa ya Kenya
4,145,000
313 /km²
Lugha mkoani Kikuyu
Kiembu
Kimeru
Mahali pa Mkoa wa Kati katika Kenya

Mkoa wa Kati (Central Province) ni mkoa wa Kenya unaoenea kati ya Mlima Kenya, Nairobi na Nyahururu. Eneo lake si kubwa lakini kuna msongamano mkubwa wa watu kulingana na mikoa ya jirani kwa sababu ya hali ya hewa na rutba ya ardhi inayolisha watu wengi. Nairobi iko nje ya mkoa.

Hali ya hewa

[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa mkoani ni poa hakuna baridi kali kutokana na kimo cha juu. Kuna mvua nyingi kiasi na majira yake ni kuanzia Machi hadi Mei halafu Oktoba hadi Novemba.

Mkoa wa Kati ni kitovu cha kilimo cha Kenya. Kuna kahawa nyingi pia mazao mengine. Maziwa na bidhaa kutokana na maziwa kama vile jibini hutengenezwa hasa mkoani. Soko zake ni pamoja na mji mkuu wa Nairobi ulio nje ya mkoa mwenyewe lakini imepakana nayo.

Makao makuuy a mkoa yapo Nyeri. Kuna wilaya saba kama zifuatazo:

Wilaya Wakazi Makao makuu
Nyandarua   479,902 Ol Kalou*
Nyeri 661,156 Nyeri
Kirinyaga 457,105 Kerugoya
Maragua 387,969 Maragua
Murang'a 348,304 Murang'a
Thika 645,713 Thika
Kiambu 744,010 Kiambu
* makao makuu ya awali: Nyahururu

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wenyeji asilia ni hasa Wagikuyu, Waembu na Wameru wanoitwa pia watu wa G.E.M.A. na kushirikiana historia ya pamoja wakitumia lugha ambazo ni karibu. Wanaaminiwa walifika mkoani katika karne ya 17.

Wakati wa ukoloni Waingereza waliona maeneo ya mkoa kufaa kwa walowezi Wazungu kutokana hali ya hewa. Hivyo sehemu kubwa zilitengwa kwa matumizi yao kwa jina la "White Highlands" (Nyanda za juu za Wazungu). Wenyeji wengi waliondolewa mashambani au walivumuliwa tu bila haki.

Siasa hii ilikuwa sababu hasa ya upinzani ulioanzishwa katika miaka ya 1940 kwa jina la Mau Mau.

Chini ya utawala wa rais Kenyatta mkoa uliona miradi mingi ya maendeleo kama barabara, viwanda na shule. Lakini wakati wa utawala wa Moi miradi mingi pamoja na barabara zilirudi nyuma.