Miguel de Cervantes
Miguel de Cervantes Saavedra (29 Septemba 1547 – 23 Aprili 1616) alikuwa mwandishi wa Hispania anayesifiwa kama mwandishi bora kabisa wa nchi yake. Mara nyingi riwaya yake "Don Quixote" [1] inahesabiwa kati ya vitabu muhimu zaidi vya fasihi ya Ulaya nzima. Riwaya hii imetafsiriwa kwenda lugha zaidi ya 140 na kuifanya kuwa kitabu kilichotafsiriwa kwa lugha nyingi zaidi duniani baada ya Biblia.
Maisha
Cervantes alizaliwa kama mtoto wa nne kati ya saba wa mganga. Hakuna habari kamili juu ya maisha yake kama kijana.
Alipokuwa na miaka 23 alijiunga na jeshi la wanamaji wa Hispania akashiriki kwenye mapigano ya Lepanto dhidi ya milki ya Osmani alipojeruhiwa na kupotewa na mkono wa kulia.
Mwaka 1575 alikamatwa na maharamia Waalgeria akawa mfungwa hadi kununuliwa na wamonaki Wakristo waliomrudisha nyumbani.
Tangu mwaka 1584 alianza kuandika lakini mwanzoni bila mafanikio ya kipesa. Alipata kazi kama mkusanyaji kodi lakini alishindwa kuonyesha hesabu safi ya mikusanyo yake akatupwa jela. Hapo alianza kazi ya kuandika riwaya yake ya "El ingenioso Hidalgo Don Quijote de la Mancha" iliyotolewa mwaka 1605 na sehemu ya pili ikafuata mwaka 1615.
Hata hivyo alikufa maskini na sifa zake zilikua baada ya kifo chake tu.
Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki. Mwaka 1613 alijiunga na Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko na tarehe 2 Aprili, siku kadhaa kabla ya kifo chake, aliweka nadhiri yake kamili.[2]
Kazi
- El ingenioso hidalgo Don Quixote de la Mancha (1605): First volume of Don Quixote.
- Novelas ejemplares (1613): mkusanyiko wa hadithi fupi 12:
- "La gitanilla" ("The Gypsy Girl")
- "El amante liberal" ("The Generous Lover")
- "Rinconete y Cortadillo" ("Rinconete & Cortadillo")
- "La española inglesa" ("The English Spanish Lady")
- "El licenciado Vidriera" ("The Lawyer of Glass")
- "La fuerza de la sangre" ("The Power of Blood")
- "El celoso extremeño" ("The Jealous Man From Extremadura")
- "La ilustre fregona" ("The Illustrious Kitchen-Maid")
- "Novela de las dos doncellas" ("The Novel of the Two Damsels")
- "Novela de la señora Cornelia" ("The Novel of Lady Cornelia")
- "Novela del casamiento engañoso" ("The Novel of the Deceitful Marriage")
- "El coloquio de los perros" ("The Dialogue of the Dogs")
- Segunda Parte del Ingenioso Cavallero [sic] Don Quixote de la Mancha (1615): Second volume of Don Quixote.
- Los trabajos de Persiles y Sigismunda (1617).
- La Galatea
Marejeo
- ↑ Tamka: ki-shot
- ↑ Fitzmaurice-Kelly, James: Miguel de Cervantes Saavedra; Oxford, Clarendon press 1913, uk. 179 na 201, online kwa archive.org
Viungo vya nje
Angalia mengine kuhusu Miguel de Cervantes kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
picha na media kutoka Commons | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
Wikisource has the text of the 1911 Encyclopædia Britannica article Cervantes Saavedra, Miguel de. |
- Works by Miguel de Cervantes katika Project Gutenberg
- Biblioteca Virtual Miguel de Cervantes (Tovuti ya Kispaniola yenye kazi zake mbalimbali ikiwemo rekodi ya kitabu cha Don Quixote
- Wahisapania maarufu
- The Cervantes Project Ilihifadhiwa 1 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Maelezo kuhusu Miguel de Cervantes
- Cervantine Collection of the Biblioteca de Catalunya Ilihifadhiwa 12 Juni 2019 kwenye Wayback Machine.
- Miguel de Cervantes (1547–1616): Wasifu waa Miguel de Cervantes Ilihifadhiwa 12 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Jumba la Makumbusho la Miguel de Cervantes Ilihifadhiwa 7 Mei 2019 kwenye Wayback Machine.
- Mkusanyiko wa kazi za Miguel de Cervantes kwenye Library of Congress
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Miguel de Cervantes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |