Nenda kwa yaliyomo

Michael Jackson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michael Jackson
Jackson mnamo 1988
Jackson mnamo 1988
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Michael Joseph Jackson
Amezaliwa (1958-08-29)29 Agosti 1958
Gary, Indiana, Marekani
Amekufa 25 Juni 2009 (umri 50)
Los Angeles, Kalifornia, Marekani
Aina ya muziki Pop, R&B, rock, soul
Kazi yake Mwimbaji, mtunzi, mtayarishaji wa rekodi, dansa, koreografa, mwigizaji, mtunzi wa vitabu, mfanyabiashara, minyamihela
Ala Sauti, Ngoma
Miaka ya kazi 1967–2009
Studio Motown, Epic, Sony
Ame/Wameshirikiana na The Jackson 5/The Jacksons
Tovuti MichaelJackson.com

Michael Joseph Jackson (29 Agosti 195825 Juni 2009) alikuwa mwimbaji, dansa na mburudishaji kutoka nchini Marekani. Hufahamika zaidi kwa jina la kiheshima-utani kama Mfalme wa Pop. Hutambulika kama mburudishaji aliyepata mafanikio zaidi kwa muda wote, na moja kati ya waburudishaji wenye mvuto na athira kubwa katika medani ya muziki. Michango yake katika muziki, dansi na fasheni,[1] na hasa suala la kuanika hadharani maisha yake binafsi, imemfanya awe kioo cha ulimwengu katika tamaduni maarufu kwa ziaidi ya miongo minne .

Akiwa pamoja na ndugu zake, Jackson amefanya uongozi wa uimbaji kwa mara ya kwanza akiwa kama mwanachama mdogo kabisa katika kundi la The Jackson 5 mnamo mwaka wa 1964. Ameanza kazi ya usanii wa kujitegemea kunako mwaka wa 1971. Albamu yake ya mwaka wa 1982 Thriller imebaki kuwa albamu yenye mauzo bora kwa muda wote. Mchango waka katika utengenezaji wa muziki wa video umeinua kutoka katika hali ya kawaida hadi katika hali ya kisanii zaidi: video zake kama vile Billie Jean, Beat It na Thriller inamfanya kuwa msanii Mmarekani Mweusi wa kwanza kupata kupigiwa nyimbo yake sana kwenye MTV. Jackson ameipa umaarufu baadhi ya maunja ya kudansi, kama vile robot na moonwalk. Staili ya muziki wake, staili ya sauti yake na zile koregrafia zilitambulika vizazi kwa vizazi, kirangi na hata katika mipaka ya kitamaduni.

Jackson ni mmoja kati ya wasanii wachache waliowekwa mara mbili kwenye Rock and Roll Hall of Fame. Mafanikio mengine yanajumlisha Guinness World Records (ikiwa ni pamoja Mburudishaji Mwenye Mafanikio kwa Muda Wote), Tuzo za Grammy 15 (ikiwa ni pamoja na ile ya Living Legend Award na ile ya Lifetime Achievement Award), 26 American Music Awards (24 akiwa kama msanii pekee ya kujitegemea, ikiwa ni pamoja na moja kwa ajili ya Msanii wa Karne)—zaidi ya msanii mwingine yeyote— single zake 17 zimeshika nafasi ya kwanza huko nchini Marekani (ikiwa ni pamoja na nne akiwa kama mwanachama wa kina Jackson 5), na inakadiriwa kafanya mauzo ya rekodi zaidi ya milioni 750 dunia nzima,[2] inafanya kuwa miongoni mwa wasanii waliouza rekodi zao vilivyo kwa muda wote na haijawahi kutokea.[3]

Maisha binafsi ya Jackson yamezua utata kwa miaka kadhaa. Kujibadilisha kwa mwonekano wake ilianza kutambulika tangu mwishoni mwa miaka ya 1970 na kuendelea, kwa kubadilisha pua yake, na rangi ya ngozi yake, imesababisha makisio kadha wa kadha katika vyombo vya habari. Mnamo mwaka wa 1993 alishtakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia kwa mtoto, ingawa hakuna mashtaka yoyote yaliyotolewa dhidi yake. Mnamo mwaka wa 2005 amejaribu kuachana na mashtaka kama yale ya awali. Ameoa mara mbili, kwanza alioa mnamo 1994 na akaja kuoa tena mnamo 1996. Amepata watoto watatu, mmoja alizaliwa kwa mama mwenye kuchukua mimba kwa ajili ya familia fulani.

Jackson amekufa mnamo tar. 25 Juni 2009 kwa kuzidisha kiasi cha dawa wakati anajiandaa na ziara ya tamasha lake la This Is It, ambalo lilitakiwa lianze katikati mwa mwaka wa 2009. Ameripotiwa kwamba alitumia dawa aina ya propofol na lorazepam. Afisa uchunguzi wa vifo wa Wilaya ya Los Angeles ameelezwa kuwa kifo chake ni uuaji wa binadamu, na mashtaka yanakwenda kwa daktari wake binafsi kwa kosa la kuua bila kukusudia. Kifo cha Jackson kimeamsha mihemko ya huzuni ulimwenguni, na huduma ya ukumbusho wake uliofanywa hadharani, ulitangazwa duniani, ulitazamwa na maelfu ya watu moja kwa moja.[4]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Michael Jackson alianza kuonekana jukwaani akiwa na miaka mitano tu pamoja na kaka na dada zake. Alitokea familia ya wanamuziki ya Jackson Five. Kuhusu miaka yake ya awali alisimulia mara kadhaa ya kwamba baba alimlazimisha kufanya mazoezi mno ya kucheza na uimbaji hivyo Michael alikosa utoto. Watazamaji wengi wamehisi ya kwamba matatizo ya kisaikolojia ya msanii yalikuwa na chanzo katika kipindi hiki.

Michael aliandika nyimbo nyingine maarufu ambazo ni 'Bad' na 'Black or White'. Huyu pia huitwa mfalme wa pop duniani.

mtoto Michael pamoja na kaka zake katika kundi la Jackson Five

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Maisha binafsi ya Michael Jackson yalikuwa yakifahamika sana. Pia, alishawahi kutiwa shaurini kwa unyanyasaji wa mtoto, lakini hakukutanika na kosa. Alifanya upasuaji maalumu ili abadilishe mwonekano wake. Michael aliyezaliwa kwa maumbile ya Mwamerika mweusi mwishoni alikuwa na ngozi nyeupe usoni na baada ya upasuaji kadhaa pua yake likawa nyembamba si pana tena. Mwenyewe alidai ya kwamba badiliko la rangi lilisababishwa na ugonjwa. Watu waliomtazama hawakupatana kama mabadiliko ya kimaumbile yalikuwa ama tokeo la kuona aibu kuonekana kama Mwafrika au jaribio kuwa na uso linalorahisisha mawasiliano yake na watu wa bara zote.

Michael, alimwoa Bi. Lisa Marie Presley, binti wa Elvis Presley. Jackson, pia alikuwa akimiliki eneo kubwa lenye makazi lililoitwa Neverland, ambalo baadaye liliuzwa kwa kampuni na nusu bado inamilikiwa na mwenyewe.

Michael Jackson amefariki mnamo tar. 25 Juni 2009 baada ya kuwaisha katika hospitali ya UCLA Medical Center.[5] Ilifikiriwa kwamba alipata mshtuko wa moyo, ikiwa na maana kwamba moyo wake ulisimama na imeonekana ya kwamba sababu yake ilikuwa matumizi mabaya ya madawa mengi mno.[6] At 4:36 pm local time, the Los Angeles coroner confirmed Jackson's death.[7]

Wakati wa umauti wake, Jackson alikuwa na umri wa miaka 50. Tetesi za habari za kifo cha Jackson, kimevunja rekodi ya mtandao na kusababisha msongamano mtandaoni[8] kwa kuwapa tabu Google, Twitter, Facebook, na Yahoo msongamano mkubwa wa utafutaji wa habari zake.[9][10]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
Albamu

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. film.com: Michael Jackson: A Fashion Retrospective, Ilihifadhiwa 1 Julai 2010 kwenye Wayback Machine. 29. Novemba 2009
  2. "Michael Jackson album sales soar". CNN. 2009-06-26. Iliwekwa mnamo 2009-09-02.
  3. Bialik, Carl (15 Julai 2009). "The Wall Street Journal, Spun: The Off-the-Wall Accounting of Record Sales by Carl Bialik, Retrieved August 21, 2009". Online.wsj.com. Iliwekwa mnamo 2 Septemba 2009.
  4. Bucci, Paul and Wood, Graeme. Michael Jackson RIP: One billion people estimated watching for gold-plated casket at memorial service Ilihifadhiwa 7 Machi 2011 kwenye Wayback Machine.. The Vancouver Sun, 7 Julai 2009.
  5. Blankstein, Andrew; Phil Willon. "Michael Jackson is dead [Updated]", The LA Times, 25 Juni 2009. Retrieved on 25 Juni 2009. 
  6. "AP: Michael Jackson Dies at Los Angeles Hospital". 25-06-2009. Iliwekwa mnamo 25-06-2009. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= na |date= (help)
  7. "Special Report with Keith Olberman", MSNBC, 25 Juni 2009. Retrieved on 2009-06-25. 
  8. http://www.usatoday.com/life/people/2009-06-26-jackson-web-traffic_N.htm
  9. http://www.pcmag.com/article2/0,2817,2349422,00.asp
  10. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-05. Iliwekwa mnamo 2009-07-02.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]