Marsupialia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Marsupialia | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mtoto mchanga wa kangaruu katika mbeleko akinyonya
|
||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Marsupiala ni ngeli ya chini ya mamalia. Ni wanayama wanaozaa wadogo wao katika hali changa sana yaani baada ya muda mfupi wa mimba. Baada ya kuzaa wanaendelea kubeba wadogo ndani ya mfuko au mbeleko ya ngozi iliyopo nje ya mwili juu ya tumbo. Humo kuna maziwa ambako wadogo wanaweza kunywa ilhali wanatunzwa vizuri na kukaa joto. Kadri wadogo wanavyokua wanaanza kutazama mazingira kutoka mbeleko na pia wanaanza kutembea nje wakirudi tena mbelekoni hadi wamefika umri wa kutosha wanaondoka.
Spishi zilizo nyingi ziko Australia na visiwa vya karibu kama New Zealand. Marsupialia wanaojulikana zaidi ni kangaruu.
Orodha ya Marsupialia [hariri]
- Bandikuti
- Kangaruu
- Koala
- Shetani wa Tasmania
- Thilasini (Chui-milia wa Tasmania)
- Oposumu
- Walabi
- Wombati
Wikimedia Commons ina media kuhusu: