Kichaa cha mbwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichaa cha mbwa
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases, veterinary medicine Edit this on Wikidata
ICD-10A82.
DiseasesDB11148
MedlinePlus001334
eMedicinemed/1374 eerg/493 ped/1974
MeSHD011818

Kichaa cha mbwa (kwa Kiingereza: rabies) ni ugonjwa hatari unaoathiri ubongo na kwa kawaida unamwua aliyeambukizwa nao.

Inatokana na ambukizo la virusi vinavyosababisha uvimbe wa ubongo (encephalytis). Virusi hivi vinaweza kutokea kwa binadamu na wanyama wa aina za mamalia na ndege [1] lakini ni mara chache kati ya wanyama wala majani. Mnyama mgugunaji ni nadra sana kuambukizwa na kichaa cha mbwa.[2]

Jina na njia za kuambukizwa[hariri | hariri chanzo]

Jina la ugonjwa linatokana na hali ya mbwa wanaoambukizwa na kuwa hatari kwa binadamu kutokana na maisha ya karibu naye. Asilimia 99 za watu huambukizwa na mbwa[2]. Lakini inatokea pia mara kwa mara kwa paka, mbweha, mbwa mwitu na wanyama wala nyama wengine, pia aina za popo, hasa huko Amerika[1][2] . Habari za maambukizo kutoka mtu mgonjwa kwenda mtu mwingine ni chache sana.[3]

Njia za maambukizo ni mate na damu kwa hiyo hasa kwa njia ya kung'atwa na mnyama mgonjwa. Mate kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa anaweza pia kusambaza kichaa cha mbwa kama mate inakuja kukutana na utando telezi wa mnyama mwingine au binadamu.[1]

Dalili za ugonjwa[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa huo inaweza tu kukutwa baada ya kuanza kwa dalili.[1] Zile za kwanza za kuambukizwa ni pamoja na homa na kuhisi mchonyoto katika eneo la mwili ambako mtu aling'atwa. [1]

Dalili hizi zinafuatwa na nyingine:

Mara dalili hizi zinapoonekana maana yake ugonjwa umeshaanza kuharibu ubongo na neva na mgonjwa hawezi kupona tena. Kifo kinafuata.

Muda kati ya kuambukizwa ugonjwa na mwanzo wa dalili ni kawaida mwezi mmoja hadi miezi mitatu. Hata hivyo, kipindi hiki kinaweza kutofautiana kutoka chini ya wiki moja hata zaidi ya mwaka mmoja.[1] Muda unategemea umbali, kwa sababu virusi lazima kusafiri kufikia mfumo mkuu wa neva kwa kufuata mishipa ya pembeni.[4]

Tiba na kinga[hariri | hariri chanzo]

Watu wanaotibiwa mara moja baada ya kuambukizwa wanaweza kupona. Lakini tiba inahitaji kutekelezwa kabla virusi havijafikia ubongo, kwa hiyo katika muda wa saa za kwanza baada ya kung'atwa. Wanyama wa kaya wanapewa chanjo dhidi ya ugonjwa huu katika nchi nyingi.

Kudhibiti wanyama na mipango ya chanjo vimepungua hatari ya kichaa cha mbwa kutoka mbwa katika nchi kadhaa.[1] Kuchanja watu kulipendekeza kwa wale walio katika hatari kubwa. Kundi hatarishi pamoja na watu wanaofanya kazi na popo au ambao hutumia muda mrefu katika maeneo ya dunia ambapo kichaa cha mbwa ni ya kawaida.[1] Katika watu hao chanjo ya kichaa cha mbwa na wakati mwingine kichaa cha mbwa immunoglobulini ina ufanisi katika kuzuia ugonjwa kama mtu anapata matibabu kabla ya kuanza kwa dalili za kichaa cha mbwa.[1]

Kuosha palipoumwa na mchukubo kwa dakika 15 kwa maji na sabuni, povidoni iodini, au sabuni vinaweza kuua virusi pia na kuwa na ufanisi fulani katika kuzuia maambukizi ya kichaa cha mbwa.[1] Ni watu wachache walionusurika maambukizi ya kichaa cha mbwa na hii ilikuwa kwa matibabu ya kina, inayojulikana kama ifataki ya Milwaukee.[5]

Uenezi[hariri | hariri chanzo]

Kichaa cha mbwa husababisha vifo vya watu wapatao 26,000 hadi 55,000 duniani kote kwa mwaka.[1][6] Zaidi ya 95% ya vifo hivi hutokea katika Asia na Afrika.[1] Kichaa cha mbwa kipo sasa katika nchi zaidi ya 150 na katika mabara yote ila Antaktika.[1] Zaidi ya watu bilioni 3 huishi katika nchi ambapo kichaa cha mbwa hutokea.[1][7][8]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 Rabies Fact Sheet N°99. World Health Organization (July 2013). Iliwekwa mnamo 28 February 2014.
  2. 2.0 2.1 2.2 Tintinalli, Judith E. (2010). Emergency Medicine: A Comprehensive Study Guide (Emergency Medicine (Tintinalli)). McGraw-Hill. pp. Chapter 152. ISBN 0-07-148480-9. 
  3. Transmission of Rabies Virus from an Organ Donor to Four Transplant Recipients (pdf)
  4. Cotran RS; Kumar V; Fausto N (2005). Robbins and Cotran Pathologic Basis of Disease (7th ed.). Elsevier/Saunders. p. 1375. ISBN 0-7216-0187-1. 
  5. Hemachudha T, Ugolini G, Wacharapluesadee S, Sungkarat W, Shuangshoti S, Laothamatas J (May 2013). "Human rabies: neuropathogenesis, diagnosis, and management.". Lancet neurology 12 (5): 498–513. PMID 23602163. doi:10.1016/s1474-4422(13)70038-3. 
  6. Lozano R, Naghavi M, Foreman K, Lim S, Shibuya K, Aboyans V, Abraham J, Adair T, Aggarwal R, et al. (Dec 15, 2012). "Global and regional mortality from 235 causes of death for 20 age groups in 1990 and 2010: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2010.". Lancet 380 (9859): 2095–128. PMID 23245604. doi:10.1016/S0140-6736(12)61728-0. 
  7. Presence / absence of rabies in 2007. World Health Organization (2007). Iliwekwa mnamo 1 March 2014.
  8. Rabies-Free Countries and Political Units. CDC. Iliwekwa mnamo 1 March 2014.