Kanaani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wakanaani walivyochorwa na Wamisri katika karne ya 13 KK.

Kanaani ni jina la zamani la eneo la Mashariki ya Kati ambalo siku hizi limegawanyika katika nchi za Israeli na Palestina, Lebanoni na sehemu za Magharibi za Jordan na Sirya.

Katika Biblia jina hilo (kwa Kiebrania כנען, knaʿn) linatumika zaidi kumaanisha sehemu ile tu ambayo ilitekwa na Waisraeli na kuitwa Israeli. Sehemu hiyohiyo baadaye tena ilikuja kuitwa pia Palestina, yaani nchi ya Wafilisti.

Baada ya mataifa hayo mawili kuteka sehemu kubwa upande wa Kusini kuanzia karne ya 13 KK, ile ya Kaskazini zaidi iliyobaki chini ya wakazi asili ilikuja kuitwa pia Foinike.

Katika eneo hilo kati ya Mesopotamia na Misri kuanzia milenia ya 4 KK ulistawi ustaarabu muhimu wa Kisemiti ambao, kati ya michango mingine, ni asili ya alfabeti.

Habari nyingi kuhusu ustaarabu huu zimejulikana hasa kwa njia ya akiolojia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.