Judi Dench

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Judi Dench

Dench at the 2007 BAFTAs
Amezaliwa Judith Olivia Dench
9 Desemba 1934 (1934-12-09) (umri 89)
York, Yorkshire, England, UK
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1957–mpaka sasa
Ndoa Michael Williams
(1971–2001) (kifo chake)

Dame Judith Olivia "Judi" Dench, CH, DBE, FRSA (amezaliwa tar. 9 Desemba 1934) ni mwigizaji filamu, weledi wa uigizaji na televisheni kutoka nchini Uingereza.

Alifanya igizo lake la kwanza mnamo mwaka wa 1957 na Old Vic Company. Miaka kadhaa iliyofuata alipata kucheza katika michezo kadhaa ya William Shakespeare - ikiwa pamoja na Ophelia kwenye Hamlet, Juliet kwenye Romeo and Juliet na Lady Macbeth kwenye Macbeth. Ameweka matawi yake rasmi kwenye kazi za filamu, na kuweza kushinda BAFTA Award akiwa Chipukizi Mwenye Mafanikio Zaidi, hata hivyo kazi zake zilizonyingi alifanya akiwa katika matamthilia. Hakufahamika sana kama mwimbaji, amechora tahakiki za nguvu kwa kazi yake akiwa kama muhusika mkuu kwenye filamu ya muziki ya Cabaret mnamo 1968.

Wakati wa makumi mawili yalifuata, akijiimalisha mwenyewe akiwa kama moja kati ya wachezaji wazuri wa tamthilia wa Kiingereza, kwa kufanya kazi na National Theatre Company na Royal Shakespeare Company. Katika televisheni, alipata mafanikio makubwa sana wakati wa kipindi hiki, kwa kushirki katika mfululizo wa A Fine Romance kuanzia 1981 mpaka 1984 na mnamo 1992 akaanza kuendelea kushiriki katika mfulizo wa kipindi cha televisheni cha kimahaba-vichekesho cha As Time Goes By .

Mionekane yake katika filamu iliendelea hadi alipokuja kuonekana mara kwa mara katika filamu za James Bond akicheza uhusika wa M kwenye GoldenEye (1995), uhusika ambao alikuwa akicheza katika James Bond tangu hapo. Amepokea tuzo kadhaa za filamu za heshima kwa uhusika wake kama Malkia Victoria kwenye Mrs. Brown (1997), na tangu hapo akaanza kuvuma sana kazi zake za katika filamu kama vileShakespeare in Love (1998), Chocolat (2000), Iris (2001), Mrs Henderson Presents (2005) na Notes on a Scandal (2006), na matayarisho ya televisheni The Last of the Blonde Bombshells (2001).

Huhesabiwa na watahakiki wengi kama mmoja kati ya waigizaji filamu wa kali wa zama-za-kivita, na baadaye kupewa jina la mwigizaji filamu wa kike-kiongozi wa Kiingereza kwa upigaji wa kura za waigizaji bora, Dench amepokea matuzo kedede kwa kazi zake uigizaji, filamu na televisheni; matuzo yake yanajumlisha BAFTAs kumi, Laurence Olivier Award saba, Screen Actors Guild Awards mbili, Golden Globe mbili, Academy Award, na Tony Award.

Aliolewa na mwigizaji Michael Williams kuanzia 1971 mpaka kiof chake mnamo mwaka wa 2001. Wao ni wazazi wa mwigizaji Finty Williams.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Dench alizaliwa mjini Heworth, York, North Riding of Yorkshire, akiwa kama binti wa Eleanora Olave (aliyekuwa Jones), mzaliwa wa Dublin, na Reginald Arthur Dench, daktari aliyekutana na mama'ke Judi wakati anasomea masuala ya afya katika Chuo cha Trinity cha mjini Dublin.[1] Dench alilelewa katika dhehebu wa Wamethodist, akiwa na umri wa miaka 13, alihitimu katika shule ya The Mount School ya mjini York, baadaye Quaker Public Secondary ikiwa ni hukohuko mjini York, na akawa Quaker.[2][3] Kaka zake, mmoja kati yao ni mwigizaji Jeffery Dench, alizaliwa mjini Tyldesley. Ndugu zake waliomaarufu ni pamoja na mpwa wake, Emma Dench, mwanahistoria wa Kiroma na profesa wa zamani katika Chuyo Kikuu cha Birkbeck huko mjini London, na sasa hivi katika Chuo Kikuu cha Harvard, Cambridge, Massachusetts.

Mnamo mwaka wa 1971, Dench ameolewa na mwigizaji filamu wa Kiingereza Michael Williams na walizaa mtoto mmoja tu mwenye jina la Tara Cressida Williams, ambaye anajulikana kisanii kama Finty Williams, aliyezaliwa mnamo tar. 24 Septemba 1972.

Dench na mume wake wamecheza pamoja katika filamu kadhaa, ikiwa pamoja na ucheshi wa Kiingereza wa Esmonde and Larbey, A Fine Romance (1981–84). Michael Williams alikuwa kwa matatizo ya kansa ya mapafu mnamo 2001, akiwa na umri wa miaka ipatayo 65.

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Staff writers. "The Importance of Dame Judi", BBC News, 6 Septemba 2002. Retrieved on 2009-02-16. 
  2. Michael Billington. "Please God, not retirement", The Guardian, 12 Septemba 2005. Retrieved on 2009-02-16. 
  3. Michael Billington. "Judi Dench: Nothing like the Dame", The Guardian, 23 Machi 1998. Retrieved on 2009-02-16. 

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: