Johnny Tri Nguyen
Johnny Tri Nguyen | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Johnny Tri Nguyen |
Alizaliwa | 16 Februari 1974 Vietnam |
Mahusiano | Ngo Thanh Van |
Johnny Tri Nguyen (kwa Kivietnam: Nguyễn Chánh Minh Trí; amezaliwa 16 Februari 1974 katika mkoa wa Binh Duong, Vietnam Kusini) ni mwigizaji wa filamu, tamthilia, "stunt" na vilevile sanaa ya mapigano wa Vietnam-Marekani.
Maisha ya awali kwa ufupi
[hariri | hariri chanzo]Johnny aliondoka nchini Vietnam akiwa na umri wa miaka 8 akiwa pamoja na familia yake, mama, baba, kaka, na dada: wote wakaelekea zao jijini Los Angeles. Johnny ni nusu Mchina kwa kuwa mama yake ni Mchina.
Familia na filamu
[hariri | hariri chanzo]Johnny Nguyen ametoka katika familia yenye asili ya uigizaji. Mjomba wake ni Nguyen Chanh Tin, mwigizaji filamu wa zamani wa Kivietnam, wakati kaka yake ni Charlie Nguyen, ambaye amewahi kuongoza filamu nyingi maarufu za kampuni ya Van Son Entertainment videos.
Shughuli za filamu kwa ufupi
[hariri | hariri chanzo]Filamu alizocheza Johnny ni kama vile Tom-Yum-Goong (ya Tony Jaa) na Cradle 2 the Grave. Kazi za ustant[1] kacheza katika filamu ya Spider-Man sehemu ya pili na alicheza kama Green Goblin katika sehemu za mwanzomwanzo. Johnny ni mtaalamu wa kupambana kwa Kung fu, Wushu , Tai chi, Aikido, na vovinam.
Filamu alizoigiza
[hariri | hariri chanzo]Filamu alizocheza kama mwigizaji
[hariri | hariri chanzo]- Nu Hon Than Chet (2008)
- Saigon Eclipse (2007)
- The Rebel (2006)
- Adventures of Johnny Tao: Rock Around the Dragon (2006)
- Hon Truong Ba Da Hang Thit (2006)
- House of the Dead 2: Dead Aim (2005)
- Tom-Yum-Goong (2005, released as The Protector in 2006)
- Demon Hunter (2005)
- House of the Dead 2: Dead Aim (2005)
- Color Blind (2005)
- Sledge: The Untold Story (2005)
- Max Havoc: Curse of the Dragon (2004)
- First Morning (2004)
- Ella Enchanted (2004)
- XMA (2004)
- The Shield (2004)
- Alias (2003)
- Cradle 2 the Grave (2003)
- The Master of Disguise (2002)
- Martial Law (1998)
Filamu alizocheza kama stant
[hariri | hariri chanzo]- The Perfect Sleep (2005)
- Jarhead (2005)
- Serenity (2005)
- Color Blind (2005)
- Ella Enchanted (2004)
- Spider-Man 2 (2004)
- Collateral (2004)
- Starship Troopers 2 (2004)
- Nudity Required (2002)
- Spider-Man (2002)
- We Were Soldiers (2002)
- Angel (1999)
- Charmed (1998)
- Mortal Kombat: Conquest (1998)
- Buffy the Vampire Slayer (1997)
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Stant ni mtu anayeigiza katika sehemu za hatari.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Akizungumzia kabila lake kwenye mahojiano na Tom-Yum-Go Ilihifadhiwa 29 Mei 2008 kwenye Wayback Machine. (WMV file))