Tamthilia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mchoro unaonyesha namna ya watu wanavyocheza tamthilia.

Tamthilia (pia: Tamthiliya au Tamthilia-Mchezo) ni moja kati ya sehemu ya utunzi wa hadithi au fasihi simulizi (ngano au hadithi) ambayo mara nyingi tunaona kupitia katika makumbi au televisheni, kusikia kupitia katika redio.

Tamthilia au mchezo mara nyingi huwa mazunguzo baina ya watu, na kwa kawaida huwa mchezo hatuutizami katika TV tu, bali hata kuna watu wengine hufuatilia kwa kupitia maandiko yenye tamthiliya hizo na kuzielewa vyema.

Watu tunaowaona wanafanya tamthilia ni waigizaji; katika ukumbi wa maonyesho husimama juu ya jukwaa na kuanza kutoa burudani huku watu wakiwaangalia (watazamaji) wanaweza wakawaona vyema kabisa.

Mwongozaji ana wasaidia waigizaji waigizaji kufanya kazi zao vyema, au anawaeleza namna ya mchezo jinsi vile unavyotakiwa kuchezwa.

Kuna aina nyingi ya michezo au tamthiliya, lakini kuna michezo sita ambayo inaonekana kuwa muhimu kupita yote:

  1. Trejidia - huu ni mchezo wa uzunu tu, kwa sababu ya mikosi na nuksi, kwa sababu ya mbabe hayuko ngangali, au kwa sababu za kimira au imani fulani.
  2. Komedia - huu unaishia na vicgekesho tu. Vitu vilivyo katika mchezo huu ni vya kuchekesha; una vunja mbavu.
  3. Domestiki drama au Igizo la kawaida - huu ni mchezo wa maisha ya kawaida, familia na marafiki.
  4. Trejikomedia - huu ni mchezo wa vitu vyote vichekesho na uzuni alkadhalika.
  5. Melodrama - huu mara nyingi unaisia na furaha. Ndani yake kunakuwa na maadui - watu wabaya - lakini mbabe hushinda. Msisiko wake una kuwa mkali sana.
  6. Simboliki - huu una husu fikra za uigizaji au mchezo. Watu wachezao katika mchezo wala sio muhimu.

Smboliki pia waweza kuitwa kwa jina la kitaalamu kama expressionistic. Ni kuhusiana zaidi na waongozaji na watunzi wakiwa wanatoa fikra zao katika mchanganuo tofauti.

Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.