Nenda kwa yaliyomo

John Maynard Keynes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John Maynard Keynes

John Maynard Keynes (5 Juni 1883 - 21 Aprili 1946) alikuwa mtaalamu wa hisabati na uchumi kutoka nchini Uingereza.

Yeye ni maarufu kwa mafundisho yake juu ya uchumi yaliyo na athira kubwa katika siasa ya kiuchumi katika nchi nyingi.

Katika nadharia yake aliandika ya kwamba uchumi wa soko huria peke yake hauelekei kumpa kila mtu kazi. Hapa alisema ya kwamba ni wajibu wa serikali kuingilia kati na kusukuma uchumi kwa kuingiza pesa katika mzunguko wa kiuchumi.