Jason Statham
| Jason Statham |
|
|---|---|
|
|
|
| Jina la kuzaliwa | Jason Statham |
| Alizaliwa | 12 Septemba 1972 Uingereza |
| Kazi yake | Mwigizaji Mwanamitindo Mwogeleaji |
Jason Statham (amezaliwa tar. 12 Septemba 1972) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Uingereza. Anafahamika zaidi kwa kucheza kama Bacon kutoka katika filamu ya Lock, Stock and Two Smoking Barrels, Jake Green kutoka katika filamu ya Revolver, Turkish kutoka katika filamu ya Snatch.
Pia Statham amepata kuonekana katika filmu nyingi sana za Kimarekani. Filamu hizo ni kama vile The Italian Job, Crank, The One na War ambazo zote alicheza na miwgizaji filamu mashuhuri wa Kichina Bw. Jet Li. Vilevile katika The Transporter, humo alicheza kama nyota kiongozi wa filamu hiyo na inaamika kwamba ile ndiyo iliyomfanya aonekane zaidi kwa watu wa Marekani.
Yaliyomo |
Wasifu[hariri]
Maisha ya awali[hariri]
Statham alizaliwa mjini Shirebrook, Derbyshire na baadaye kuhamia mjini London. Ni mtoto wa pili wa wazazi ambao mmoja wao alikuwa mwimbaji na mwingine mwundaji wa nguo. Alikulia katika maisha ya kimichezo na ni mwogeleaji mzuri - mwanariadha. Na amewahi kushinda mashindano ya kimataifa ya mbio kwa mwaka wa 1992.[1] Vilevile amewahi kuwa mwanachama wa Kikosi cha Waogeleaji cha Taifa cha Britain kwa takriban miaka kumi na miwili. Pia Statham ni mtaalam wa martial arts na Kick Boxing.
Mainsha binafsi[hariri]
Statham amewahi kuwa mahusiano ya kimapenzi na mwigizaji filamu-mwanamitindo wa Kiingereza Bi. Kelly Brook kwa takriban miaka saba, lakini wakaja kutengana pale mwanamama Kelly alipokutana na mwigizaji filamu mwenzi Bw. Billy Zane wakati wa kucheza filamu ya Survival Island na kupelekea kuwa mpenzi wa mwigizaji huyo. Mnamo mwaka wa 2005, Statham akaanzisha mahusiano na mwimbaji wa zamani Bi. Sophie Monk, lakini mapenzi yao hayakudumu sana wakaachana.
Filamu alizocheza[hariri]
| Mwaka | Jina la filamu | Jina alilotumia | Maelezo |
|---|---|---|---|
| 1998 | Lock, Stock and Two Smoking Barrels | Bacon | |
| 2000 | Snatch | Turkish | |
| Turn It Up | Mr. B | ||
| 2001 | Ghosts of Mars | Sgt. Jericho Butler | |
| The One | MVA Agent Evan Funsch | ||
| Mean Machine | Monk | ||
| 2002 | Thai Boxing: A Fighting Chance | Narrator | |
| The Transporter | Frank Martin | ||
| 2003 | The Italian Job | Handsome Rob | |
| 2004 | Collateral | Airport Man | Cameo appearance |
| Cellular | Ethan Greer | ||
| 2005 | Transporter 2 | Frank Martin | |
| Revolver | Jake Green | ||
| London | Bateman | ||
| 2006 | Chaos | Detective Quentin Conners | |
| The Pink Panther | Yves Gluant | Uncredited role | |
| Crank | Chev Chelios | ||
| 2007 | War | FBI Agent John Crawford | |
| In the Name of the King: A Dungeon Siege Tale | Farmer Daimon | ||
| 2008 | The Bank Job | Terry Leather | |
| Death Race | Frankenstein | awaiting release | |
| 2009 | Transporter 3 | Frank Martin | filming |
| Crank 2: High Voltage | Chev Chelios | filming |
Marejeo[hariri]
- ↑ An interview with Jason Statham at IGN.com