Irmina wa Trier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Irmina.

Irmina wa Trier (Trier, leo nchini Ujerumani, karne ya 7; Wissembourg, leo nchini Ufaransa, 716) alikuwa mwanamke wa ukoo wa kifalme ambaye, labda baada ya kuolewa na kuzaa watoto watano[1], alianzisha monasteri huko Oehren akaiendesha kama abesi hadi kifo chake[2].

Alimfadhili sana Wilibrodi katika umisionari wake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Desemba[3]..

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Christian Settipani, Les Ancêtres de Charlemagne, Paris, Société atlantique d'impression, 1989, 170 p. ISBN 2-906483-28-1.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/82950
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.