Elimu kwa watoto wa kike
Mandhari
Elimu ni kitu muhimu kwa maisha ya sasa kwa kila mtu: awe mwanamke au mwanamume inampasa kupata elimu ili aweze kumsaidia maishani. Lakini duniani hadi siku hizi watoto wa kike wanakosa au wananyimwa haki ya kupata elimu.
Tatizo hilo ni kubwa zaidi katika mabara ya Afrika na Asia ambapo watoto wa kike wanakosa elimu kutokana na mila potofu za mataifa hayo. Si hivyo tu: wanakosa elimu ila wanalazimishwa kuolewa wakiwa wadogo na hawawezi kulea familia; ndiyo maana hali ya maisha katika mabara hayo si nzuri. Kumbe elimu kwa watoto wa kike ni haki yao ya msingi.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elimu kwa watoto wa kike kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |