Dennis Oliech
Dennis Oliech | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Dennis Oliech | |
Tarehe ya kuzaliwa | 2 Februari 1985 | |
Mahala pa kuzaliwa | Nairobi, Kenya | |
Nafasi anayochezea | Mshambuliaji | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | AJ Auxerre | |
Namba | 14 | |
Klabu za vijana | ||
Mathare United | ||
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
2007 | AJ Auxerre | |
Timu ya taifa | ||
2006 | Kenya | |
* Magoli alioshinda |
Dennis Oliech (amezaliwa Nairobi, Kenya, 2 Februari 1985) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchi ya Kenya, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya AJ Auxerre katika Ligi ya kwanza ya Ufaransa. Ligi hiyo hujulikana zaidi kwa jina la Ligue 1.
Kucheza katika timu ya taifa
[hariri | hariri chanzo]Oliech alianza kuichezea Timu ya taifa ya soka ya Kenya tarehe 4 mei 2002.
Alianza kucheza mpira katika umri wake mdogo katika klabu ndogo huko Kenya iitwayo Dagoretti Santos, baada ya hapo akajiunga na klabu mashuhuri Kenya Mathare United.
Oliech baadae alitokea kua mfungaji mabao wakutegemewa katika Timu ya Taifa ya Kenya mashuhuri kwa jina la Harambee Stars kwa kila mechi nyingi za taifa alikua akifunga magoli. Ni mchezaji aliyeingia katika kipindi cha pili na alifunga goli la kusaidia Kenya ili kupata tiketi ya kuingia katika Kombe la Mataifa ya Afrika na mechi hiyo ilikua ni ya mwisho dhidi ya Cabo Verde. Alicheza katika Kombe la Mataifa ya Afrika huko Tunisia mwaka 2004. Na huo mwaka ndio alichaguliwa kua miongoni mwa wachezaji chipukizi bora wenye kipaji pamoja na Wayne Rooney wa Manchester United
Alianza kucheza mechi ya kimataifa katika Timu ya Taifa ya Kenya na ilikua dhidi ya timu ya Nigeria na mechi hiyo walifungwa 3-0.
Kutoka nje ya Kenya
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2003 baada ya kuonekana mchezaji mzuri, klabu aina mbali mbali zilipendelea kumnunua lakini mchezaji huyo aliamua kujiunga na klabu ya Qatar iitwayo Al-Arabi na aliichezea hadi mwaka 2005. Katika mwaka 2004 nchi ya Qatar ilimpka Ksh 200 milioni ili kubadili uraia nakuchukua uraia wa Qatar lakini alikataa. Wapenzi wake huko Kenya walifurahi sana baada ya yeye kukataa kuchukua uraia huo na akachukuliwa kua ni mtu anayependa nchi yake kuliko pesa.
Kucheza Ufaransa
[hariri | hariri chanzo]Baada ya hapo Oliech alipata fursa ya kujiunga na klabu ya FC Nantes katika Ligi ya kwanza (Ligue 1) mwaka 2005, lakini alianza kuichezea hiyo klabu vizuri mwaka 2006, mwaka 2007 klabu hiyo ya FC Nantes iliporomoka Ligi ya pili(Ligue 2) baada ya kukokota mkia katika ligi ya kwanza. Oliech aliuzwa kwakuazimwa katika klabu ya AJ Auxerre ambayo ilikua inahitaji mshambuliaji wakuisaidia kufunga mabao baada ya timu hiyo kuanza vibaya katika Ligi ya kwanza ya Ufaransa katika msimu wa 2007.
Katika Januari 2007 AJ Auxerre ilimnunua moja kwa moja kutoka FC Nantes.
Kurudi Kenya
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2018 alisajili na moja wapo wa timu za Kenya almaarufu Gor Mahia kwa kima cha nusu milioni baada yake kustaafu kuichezea timu ya taifa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Mchezaji huu katika Tovuvi rasmi ya Ligi ya Kwanza ya Ufaransa
- Katika Tovuti maarufu ya koora Kiingereza
- Katika Tovuti maarufu ya koora Kiarabu
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dennis Oliech kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |