Cody Gakpo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha inamuonyesha Cody Gakpo akiwa PSV Eindhoven chini ya miaka 19.

Cody Mathès Gakpo (alizaliwa 7 Mei 1999) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Uholanzi ambaye anacheza katika nafasi ya mshambuliaji katika klabu kongwe Uingereza ya Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi. [1]

Mhitimu wa akademi ya PSV, Gakpo alicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza mnamo Februari 2018. Katika msimu wa 2021-22, alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Uholanzi baada ya kufunga mabao 21 katika michezo 47 katika mashindano yote. Alisajiliwa na Liverpool Januari 2023.

Gakpo aliichezea Uholanzi katika michuano ya kimataifa ya vijana wa chini ya umri wa miaka 18, na hadi kuichezea katika umri wa chini ya miaka 21. Alipata nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mnamo Juni 2021 kwenye UEFA Euro ya mwaka 2020.

Maisha yake ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Gakpo alizaliwa Eindhoven na kukulia katika wilaya ya Stratum.[2] Baba yake alizaliwa Togo na ana asili ya Ghana, wakati mama yake ni Mholanzi.[3][4][5] Mnamo mwaka 2007, alihamia katika akademi ya vijana ya PSV, ambapo aliendeleza kipaji chake cha mpira na kucheza katika timu zote za vijana.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Squad List: FIFA World Cup Qatar 2022: Netherlands (NED)". FIFA. 18 December 2022. uk. 20. Iliwekwa mnamo 1 January 2023.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Cody Gakpo: van Stratum naar de spotlights", 9 October 2019. (nl) 
  3. 3.0 3.1 "Cody Gakpo leeft de droom van bijna elke Eindhovense jongen", 1 June 2019. (nl) 
  4. "Ghana coach reveals talks with Dutch players", 17 October 2019. 
  5. "EXCLUSIVE: Ghanaian sensation Cody Gakpo extends contract with Dutch giants PSV Eindhoven", 12 September 2019. Retrieved on 2023-03-09. Archived from the original on 2019-11-09. 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cody Gakpo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.