Coahuila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Saltillo, Coahuila
Bendera ya Coahuila
Mahali pa Coahuila katika Mexiko

Coahuila (jina rasmi: Coahuila de Zaragoza) ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kaskazini ya nchi. Mji mkuu na mji mkubwa ni Saltillo. Jimbo lina wakazi wapatao 2,495,200 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 149,982.

Imepakana na Marekani (Texas), Nuevo León, Zacatecas, San Luis Potosí, Durango na Chihuahua. Kuna jumuiya pili katika Coahuila: Wazungu ambao ni 74% ya wakazi wote na wamestizo ni 20% ya wakazi.

Gavana wa jimbo ni Humberto Moreira Valdés.

Lugha rasmi ni Kihispania.

Miji Mikubwa[hariri | hariri chanzo]

  1. Saltillo (633,667)
  2. Ciudad Acuña (209,000)
  3. Monclova (200,160)
  4. Piedras Negras (143,915)



Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]



Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Coahuila kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.