Bustani ya wanyama ya Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bustani ya wanyama wa Dar es Salaam ni bustani ya wanyama iliyopo Dar es Salaam, Tanzania. Bustani iko katika wilaya ya Kigamboni upande wa mashariki wa jiji, km 37 kutoka katikati ya Dar es Salaam.[1]

Vivutio[hariri | hariri chanzo]

Mbuga ya wanyama ya Dar es Salaam inajulikana zaidi kwa kuwa na wanyama wengi nchini Tanzania, wakiwemo pundamilia, mamba, swala, kobe, nyani, fisi, simba, chui, nyoka na aina kadhaa za ndege. Pia kuna eneo la watoto la michezo. Zoo ya Dar es salaam pia ina bwawa la kuogelea la watoto na vijana chini ya miaka 13. Zoo ya Dar es salaam inatoa fursa kwa wageni na wenyeji kuwa karibu na wanyama na kuingiliana na baadhi ya wanyama mfano nyani, farasi, punda na ngamia, pia kutoa safari ya ndoto kwa wageni. Mto Nguva pia ni moja ya vivutio vikubwa vya Zoo ya Dar es salaam, ukitoa maji na hali ya hewa ya baridi kwa uoto wa asili unaovutia aina mbalimbali za ndege wa rangi na wa kuvutia, vipepeo na viumbe vingine vya asili vya urembo. Ni mojawapo ya mbuga kubwa zaidi za wanyama katika Afrika Mashariki hivyo kutoa ladha yake ya kipekee kwa wenyeji na wageni.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Dar Es Salaam Zoo". ZoomTanzania.