Buganivilia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Buganivilia | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bougainvillea spectabilis
|
||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Buganivilia ni jenasi la mimea waotao maua yenye asili yao katika Bara la Marekani Kusini kuanzia Brazili na kusonga magharibi kuelekea Peru na kusini hadi Argentina kusini (Mkoa wa Chubut).
Waandishi tofauti wanakubali kuwa kuna kati ya spishi 4 na 18 za jenasi hii. Mmmea huu uligunduliwa nchini Brazili mnamo mwaka wa 1768, na Philibert Commerçon, Msomi wa mimea kutoka nchi ya Ufaransa alipokuwa akimwandama mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Kifaransa na mpelelezi Louis Antoine de Bougainville wakati wa safari yake ya kuizunguka Dunia.