Birmingham Post
| Birmingham Post | |
|---|---|
| Jina la gazeti | Birmingham Post |
| Aina ya gazeti | *. Gazeti la kila wiki |
| Lilianzishwa | 1857 |
| Nchi | Uingereza |
| Mwanzilishi | John Frederick Feeney |
| Mhariri | Alun Thorne |
| Mmiliki | Trinity Mirror |
| Makao Makuu ya kampuni | Birmingham |
| Nakala zinazosambazwa | 12,550 (Jan-Jun 2006)[1] |
| Tovuti | http://www.birminghampost.net |
Birmingham Post ni gazeti lililoanza kuchapishwa hapo awali chini ya jina la Daily Post katika eneo la Birmingham, Uingereza katika mwaka wa 1857 na John Frederick Feeney. Hili lilikuwa gazeti liuzwalo sana katika eneo la West Midlands, ingawaje haikuwa na ushindani kutoka magazeti mengine katika eneo hili. Mtindo wa kuchapisha ilibadilishwa katika mwaka wa 2008. Gazeti hili liliacha kuchapisha mwatangazo katika ukurasa wake wa kwanza katika mwaka wa 1946 na likaanza kuchapisha habari muhimu katika ukurasa huo wa kwanza.
Jengo la Post and Mail katika mji wa Birmingham lilifunguliwa katika mwaka wa 1965 ili kutumikia magazeti ya Post na Evening Mail lakini Post na magazeti dada yake yalihamia jengo la Fort Dunlop, maili tatu kutoka katikati wa mji, katika mwezi wa Agosti 2008.
Baada ya usimamizi kubadilika mara kadhaa, gazeti hilo ni kampuni shirika katika kundi la Trinity Mirror Group. Mnamo Februari 2008, gazeti hilo lilianzisha tovuti yake upya kama birminghampost.net.
Mnamo Novemba 2009, jarida lilianza kuchapishwa kila wiki badala ya kila siku.
[hariri] Marejeo
- ^ Birmingham Post (Mon-Sat) Standard Certificate of Circulation, 02-Jan-2006 to 02-Jul-2006 Audit Bureau of Circulations
- ^ Manchester Guardian changes - The Guardian (republished by Guardian Unlimited Archives), Septemba 27, 1952
- ^ Paul Dale, "Editor Marc Reeves slays some sacred cows as Birmingham Post goes weekly", Birmingham Post, 6 Novemba 2009