Ambrosio Fransisko Ferro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maziara ya wafiadini wa Natal.

Ambrosio Fransisko Ferro (alizaliwa funguvisiwa la Azori, Ureno - alifariki Cunhaú, Brazil, 3 Oktoba 1645) alikuwa paroko wa Natal, Brazil wakati wa ukoloni.

Aliuawa kikatili na Waprotestanti pamoja na waumini 27 wakati wa kuadhimisha Misa kanisani[1].

Padri mwingine, Andrea wa Soveral, na wenzake 69 walikuwa wameshauawa vilevile tarehe 16 Julai mwaka uleule.

Papa Yohane Paulo II aliwatangaza wenye heri tarehe 5 Machi 2000, halafu Papa Fransisko aliwatangaza watakatifu tarehe 15 Oktoba 2017[2].

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Julai[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.