James Omingo Magara
James Omingo Magara ni mwanasiasa wa Kenya. Kwa sasa yeye ni Mwanachama wa Orange Democratic Movement na alichaguliwa kuwa mbunge wa Mugirango Kusini katika uchaguzi wa 2007. Alishinda kiti hiki mara ya kwanza kwa tiketi ya FORD-Kenya katika uchaguzi mdogo mnamo 2001, akichukua nafasi ya nduguye marehemu Enock Nyakieya Magara aliyefariki katika ajali ya gari[1]
Alihifadhi kiti chake katika Uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2002, wakati huu akiwakilisha chama cha Ford People[2] na pia katika Uchaguzi wa 2007, akiwakilisha Chama cha ODM[3]
Uwaziri[hariri | hariri chanzo]
Tangu kuchaguliwa amewahi kuwa Naibu wa Waziri wa biashara. Hata hivyo, mnamo Desemba,2009, Mahakama kuu ya Kenya ilitangaza kiti cha Ubunge cha Mugirango Kusini wazi kutokana na udanganyifu katika uchaguzi, ingawa Magara mwenyewe hakupatikana na hatia ya udanganyifu[4]
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
Virejeleo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Daily Telegraph, 3 Agosti 2009: news/africaandindianocean/kenya/1336285/Dismissed-minister-shot-dead-in-Kenya.html Waziri auawa nchini Kenya[dead link]
- ↑ Mfumo wa Vyama vingi: Siasa na Wabunge nchini Kenya 1944-2007[dead link]
- ↑ Wabunge wa Bunge la 10 Archived 17 Juni 2008 at the Wayback Machine.. Bunge la Kenya, lililopatikana 19 Juni 2008
- ↑ Daily Nation, 17 Desemba 2009: Magara Apoteza Kiti cha Mugirango Kusini
Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]
Ford Kenya Uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2002 Wabunge wa Kenya Mugirango Kusini
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu James Omingo Magara kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |