James Omingo Magara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
James O. Magara

James Omingo Magara ni mwanasiasa wa Kenya. Kwa sasa yeye ni Mwanachama wa Orange Democratic Movement na alichaguliwa kuwa mbunge wa Mugirango Kusini katika uchaguzi wa 2007. Alishinda kiti hiki mara ya kwanza kwa tiketi ya FORD-Kenya katika uchaguzi mdogo mnamo 2001, akichukua nafasi ya nduguye marehemu Enock Nyakieya Magara aliyefariki katika ajali ya gari[1]

Alihifadhi kiti chake katika Uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2002, wakati huu akiwakilisha chama cha Ford People[2] na pia katika Uchaguzi wa 2007, akiwakilisha Chama cha ODM[3]

Uwaziri[hariri | hariri chanzo]

Tangu kuchaguliwa amewahi kuwa Naibu wa Waziri wa biashara. Hata hivyo, mnamo Desemba,2009, Mahakama kuu ya Kenya ilitangaza kiti cha Ubunge cha Mugirango Kusini wazi kutokana na udanganyifu katika uchaguzi, ingawa Magara mwenyewe hakupatikana na hatia ya udanganyifu[4]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Ford Kenya Uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2002 Wabunge wa Kenya Mugirango Kusini

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Omingo Magara kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.