Koikoi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Koikoi
Koikoi kijivu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Pelecaniformes (Ndege kama wari)
Familia: Ardeidae (Ndege walio na mnasaba na koikoi)
Jenasi: Ardea (Koikoi)
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 12:

Koikoi ni ndege wakubwa wa jenasi Ardea katika familia ya Ardeidae wenye miguu mirefu na domo refu na nyembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, kijivu na nyeusi. Spishi zenye rangi ya kahawiachekundu huitwa pondagundi pia. Spishi nyingine nyeupe kabisa inaitwa msuka. Zamani ilikuwa imeainishwa ndani ya jenasi Egretta. Koikoi hupenda kula samaki lakini hula wanyama wadogo pia, kama vyura, mijusi, nyoka na panya. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia[hariri | hariri chanzo]

  • Ardea bennuides (Bennu Heron)
  • Ardea formosa
  • Ardea howardae
  • Ardea polkensis (Mwanzo wa Pliocene ya Bone Valley, MMA)
  • Ardea similis
  • Ardea sp. (Kati ya Miocene ya Observation Quarry, MMA)
  • Ardea sp. (Mwisho wa Miocene ya Love Bone Bed , MMA)
  • Ardea sp. (Mwanzo wa Pleistocene ya Macasphalt Shell Pit, MMA)

Picha[hariri | hariri chanzo]