Koikoi
Mandhari
(Elekezwa kutoka Pondagundi)
Koikoi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Spishi 12:
|
Koikoi ni ndege wakubwa wa jenasi Ardea katika familia ya Ardeidae wenye miguu mirefu na domo refu na nyembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, kijivu na nyeusi. Spishi zenye rangi ya kahawiachekundu huitwa pondagundi pia. Spishi nyingine nyeupe kabisa inaitwa msuka. Zamani ilikuwa imeainishwa ndani ya jenasi Egretta. Koikoi hupenda kula samaki lakini hula wanyama wadogo pia, kama vyura, mijusi, nyoka na panya. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti. Jike huyataga mayai 2-6.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Ardea alba, Msuka (Great White Egret)
- Ardea a. alba, Msuka wa Ulaya (Eurasian Great White Egret)
- Ardea a. melanorhynchos, Msuka wa Afrika (African Great White Egret)
- Ardea cinerea, Koikoi Kijivu (Grey Heron)
- Ardea c. cinerea, Koikoi Kijivu (Grey Heron)
- Ardea c. firasa, Koikoi Kijivu wa Visiwa (Indian Ocean Grey Heron)
- Ardea goliath, Pondagundi Mkubwa au Koikoi Jitu (Goliath Heron)
- Ardea humbloti, Koikoi wa Madagaska (Humblot's Heron)
- Ardea intermedia, Koikoi domo-njano (Intermediate Heron)
- Ardea i. brachyrhyncha, Koikoi domo-njano (Yellow-billed Heron)
- Ardea melanocephala, Koikoi Majoka (Black-headed Heron)
- Ardea purpurea, Pondagundi (Purple Heron)
- Ardea p. bournei, Pondagundi wa Kaboverde (Cape Verde Purple Heron)
- Ardea p. madagascariensis, Pondagundi wa Madagaska (Madagascar Purple Heron)
- Ardea p. purpurea, Pondagundi (Purple Heron)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Ardea cocoi (Cocoi Heron)
- Ardea herodias (Great Blue Heron)
- Ardea insignis (White-bellied Heron)
- Ardea pacifica (White-necked or Pacific Heron)
- Ardea picata (Pied Heron)
- Ardea sumatrana (Great-billed Heron)
Spishi za kabla ya historia
[hariri | hariri chanzo]- Ardea bennuides (Bennu Heron)
- Ardea formosa
- Ardea howardae
- Ardea polkensis (Mwanzo wa Pliocene ya Bone Valley, MMA)
- Ardea similis
- Ardea sp. (Kati ya Miocene ya Observation Quarry, MMA)
- Ardea sp. (Mwisho wa Miocene ya Love Bone Bed , MMA)
- Ardea sp. (Mwanzo wa Pleistocene ya Macasphalt Shell Pit, MMA)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Msuka
-
Koikoi kijivu
-
Pondagundi mkubwa
-
Koikoi wa Madagaska
-
Koikoi domo-njano
-
Koikoi majoka
-
Pondagundi
-
Cocoi heron
-
Great blue heron
-
White-bellied heron
-
White-necked heron
-
Pied heron
-
Great-billed heron