Nenda kwa yaliyomo

Albatrosi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Albatrosi
Albatrosi utosi-mweupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Procellariiformes (Ndege kama walinzi)
Familia: Diomedeidae (Ndege walio na mnasaba na albatrosi)
Gray, 1840
Ngazi za chini

Jenasi 4:

Albatrosi (kutoka Kiing.: albatross) ni ndege wakubwa wa bahari katika familia Diomedeidae. Baina ya spishi hizi yuko ndege wenye mabawa marefu kabisa kuliko ndege wote duniani. Albatrosi Mlizi ana mabawa ambayo mawili pamoja yana urefu wa sm 310 kwa wastani na urefu mkubwa kabisa uliopimwa ulikuwa sm 370. Rangi zao zinatofautiana kutoka nyeupe na mabawa kijivu hafifu hadi mwili wote kijivucheusi. Wana domo kubwa sana lenye ncha kwa umbo la kulabu. Mirija miwili ya pua inapitia pande zote mbili za domo.

Ndege hawa huenda mbali sana wakiruka angani na wanaweza kuzunguka dunia. Hawapigi mabawa sana baada ya kuruka, lakini wananyiririka kwa mabawa yaliyonyooshwa. Huwakamata ngisi, samaki na gegereka na hula mizoga pia. Kwa kawaida albatrosi huyatengeneza matago yao kwenye visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Kabla ya kujamiiana dume na jike hutenga dansi ya kanuni kaida. Jike hulitaga yai moja tu.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]