Nenda kwa yaliyomo

Yagazie Emezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yagazie Emezi
Nchi Nigeria
Majina mengine Emezi
Kazi yake Mpiga picha


Yagazie Emezi ni mpigapicha wa Nigeria.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Emezi alizaliwa na kukulia katika jimbo la Aba, Nigeria na ni kitinda mimba katika familia ya watoto wawili.

Yagazie Emezi alianza kazi ya upigaji picha mwaka 2015 na amekua akifanya kazi kwa makampuni ya ‘’The Washington’’, ‘’National Geographic’’,[1] ‘’Al-Jazeera’’, ‘’The New York Times’’, ‘’Vogue’’, ‘’Newsweek’’, ‘’Inc. Magazine’’, ‘’Time magazine’’, ‘’The Guardian’’, ‘’Refinery29’’, ‘’Everyday Projects’’, na ‘’The Weather Channel’’.[2] Mnamo mwaka 2017, Yagazie aliishi Monrovia, Liberia kwa miezi kumi akifanya uandishi juu ya athari ya elimu kwa wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi na baadaye alirudi kuendelea na kazi yake ya awali kwa jina la ‘’Re-learning Bodies’’ inayofuatilia ni kwa namna gani waliopatwa na kiwewe kuachana na zilizotokana na vurugu na unyanyasaji wanavyobadilika na kutoa alama juu ya ukosekanaji wa utamaduni chanya kuuzunguka mwili Pamoja na mambo muhimu katika Nyanja za tamaduni. Yagazie alipokea tuzo za mwaka za 2018 katika kipengele cha ubunifukutoka Getty Images, alishiriki pia katika marejeo ya jijini New York mwaka 2018. Ameshirikishwa pia na majarida ya picha ya nchini Uingereza kama, ‘’Huffington Post’’, ‘’i-D’’, ‘’Nieman Reports’’, ‘’Paper Magazine’’, ‘’Vogue’’, ‘’CNN’’ na ‘’The Washington Post’’. Mwaka 2018, alipata ruzuku kutoka ubalozi wa Marekani nchini Nigeria kutokana na mfululizo wa picha zake zinazoonyesha uhalisia wa manyanyaso ya ngono kwa wanawake na Watoto jijini, Nigeria. Mwaka 2019, akawa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika kufanya kazi katika jarida la ‘’National Geographic Magazine’’ na pia anafaidi ruzuku kama mtafiti wa ‘’National Geographic’’. Yagazie alikua miongoni mwa wasanii walioteuliwa mwaka 2019 kushiriki maonyesho ya Sanaa ya Kehinde Wiley huko Black Rock, Senegal. Picha yake ililenga kupinga hali ya kisiasa ya nchini Nigeria.

Emezi alipata teuzi katika tuzo za mwaka 2019 kwa jina la ‘’Rolex Mentor and Protégé Arts Initiative’’. Anahudumu katika bodi ya washauri ya ‘’Everyday Africa’’[3] na pia ni mwanachama anayechangia.

Maongezi

[hariri | hariri chanzo]
  • 2019 Mabadiliko ya kimazingira & Hatarishi kwa afya za wanawake,[4]Muongeaji, University of Global Health Equity, Kigali, Rwanda
  • 2019 Namna gani Sanaa inaweza kuchangia matokeo chanya katika afya, Muongeaji, Hamwe Festival. Kigali, Rwanda[5]
  • 2019 Hali iliyo sugu: Kutambua, kuona na kuponya miili katika Afrika kwa ujumla,[6] Muongeaji, chuo kikuu cha Kansas. Kansas, Marekani
  • 2018 Kwenda kwa kasi: wanawake katika tasnia ya picha, Muongeaji, maonyesho ya picha ya Lagos. Lagos, Nigeria
  • 2018 Mhadhiri mualikwa, Muongeaji, New York, Marekani
  • 2017 Kufikiri tena juu ya uumbaji katika karne ya sasa, Muongeaji, FCAEA & Everyday Africa. Nairobi, Kenya,
  • 2016 Simulizi kupitia picha, Muongeaji, wiki ya mitandao ya kijamii. Lagos, Nigeria.
  • 2015 Changamoto ya kuchunguza picha nje ya mitaa, Muongeaji. Lagos, Nigeria.
  • 2015 Kuunganishwa na watumiaji, kitu gani tunajua na jinsi ya kukitumia, Muongeaji,. Lagos, Nigeria.

Tuzo na Ruzuku

[hariri | hariri chanzo]
  • National Geographic 2020 mfaidi wa zuruku.[7]
  • Mshindi wa tuzo za mwaka 2018 za Getty Images.[8][9]
  • Zuruku kutoka ubalozi wa Marekani nchini Nigeria mwaka 2018.
  • Tuzo maalum ya wahitimu wa chuo cha new Mexico ‘’University of New Mexico’’ mwaka 2017, Idara ya mafunzo ya Afrika.

Maonyesho

[hariri | hariri chanzo]
  • African Biennale of Photography, Bamako, Mali. 2019.[10]
  • The Female Lens, makumbusho ya picha ya Richard Taittinger, New York, Marekani. 2019
  • Relearning Bodies, sherehe za Hamwe, Kigali, Rwanda. 2019
  • HERE, ‘’Alliance française’’, Lagos, Nigeria. 2019
  • Present and Forgotten, ‘’Visco Corporation|Vlisco&Co’’, Art Twenty One. Lagos, Nigeria. 2018
  • Festival Pil’ours, Saint Gilles Croix de Vie, France. 2018
  • Insider/Outsider, Women Photograph, Photoville. New York, Marekani. 2017
  • Body Talk, Refinery29, Photoville. New York, Marekani, 2017
  • Re-picturing a Continent, Alliance Francais, Everyday Africa. Nairobi, Kenya. 2017
  • LOOK3 Festival of the Photograph, Charlottesville, Marekani. 2016
  • The Everyday Projects at FotoIstanbul, Istanbul, Turkey. 2016
  1. "How women are stepping up to remake Rwanda". Culture (kwa Kiingereza). 2019-10-15. Iliwekwa mnamo 2020-06-13.
  2. "Exodus: The Climate Migration Crisis". YAGAZIE EMEZI. Iliwekwa mnamo 8 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "About". YAGAZIE EMEZI (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-06-13.
  4. "Andrew W. Mellon Foundation Sawyer Seminar". The University of Kansas (kwa Kiingereza). 2019-08-28. Iliwekwa mnamo 2020-06-13.
  5. "Hamwe Talks". UGHE (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-06-13.
  6. "Andrew W. Mellon Foundation Sawyer Seminar". The University of Kansas (kwa Kiingereza). 2019-08-28. Iliwekwa mnamo 2020-06-13.
  7. "Explorers Directory". www.nationalgeographic.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-13. Iliwekwa mnamo 2020-06-13.
  8. BellaNaija.com (Januari 30, 2018). "Yagazie Emezi receives{sic) inuagural Creative Bursary Award from Getty Images". BellaNaija. Iliwekwa mnamo 8 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Nigerian Photographer Yagazie Emezi wins Getty Images Award". Punch Newspapers. Iliwekwa mnamo 8 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Bamako Encounters". www.e-flux.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-06-13.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yagazie Emezi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.