Nenda kwa yaliyomo

William Plomer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

William Charles Franklyn Plomer (10 Desemba, 1903 - 21 Septemba, 1973) alikuwa mwandishi wa Afrika Kusini na Uingereza. Hasa aliandika riwaya, hadithi fupi na mashairi.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Plomer alizaliwa tarehe 10 Desemba, mwaka wa 1903 mjini Pietersburg nchini Afrika Kusini. Mamake angependelea kuishi Uingereza lakini babake alipendelea Afrika Kusini, na kwa vyovyote walikuwa hawana pesa za kutosha kuishi Uingereza. Kwa hiyo, Plomer alisomeshwa Johannesburg. Alipohitimu sekondari alifanya kazi katika kilimo kabla hajawa mwandishi; riwaya yake ya kwanza ilitolewa mwaka wa 1925. Mwaka wa 1926 alimuunga mkono Roy Campbell kuanzisha gazeti la Voorslag lakini wafadhili wao wakawanyima pesa kwa ajili ya maoni yao ya kisiasa. Plomer akahamia Ujapani ambako alikuwa mwalimu kwa miaka mitatu. Mwaka wa 1929 akahamia Uingereza ambako aliishi hadi mwisho wa maisha yake akiwa anaendelea kufanya kazi kama mwandishi na mhariri.

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Riwaya[hariri | hariri chanzo]

 • Turbott Wolfe (1925)
 • Sado (1931)
 • The Case is Altered (1932)
 • The Invaders (1934)
 • Museum Pieces (1952)

Hadithi Fupi[hariri | hariri chanzo]

 • I Speak for Africa (1927)
 • Paper Houses (1929)
 • The Child of Queen Victoria (1933)
 • Curious Relations (1945)
 • Four Countries (1949)

Mashairi[hariri | hariri chanzo]

 • Notes for Poems (1927)
 • The Family Tree (1929)
 • The Fivefold Screen (1932)
 • Visiting the Caves (1936)
 • The Dorking Thigh (1945)
 • A Shot in the Dark (1955)
 • A Choice of Ballads (1960)
 • Taste and Remember (1966)
 • Celebrations (1972)

Mengine[hariri | hariri chanzo]

 • Cecil Rhodes (1933)
 • Ali the Lion (1936)
 • Double Lives: An Autobiography (1943)
 • At Home: Memoirs (1958)
 • Conversation with My Younger Self (1963)

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 • Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN: 1-86914-028-1
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu William Plomer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.